Habari Kali
Loading...

WAMACHINGA WAMUUA ASKARI JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KUMPIGA NA STULI KICHWANI.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
 
Mke wa Marehemu Stephano Benjamin (katikati) akisaidiwa na jamaa wa karibu msibani kumuaga marehemu mume wake.

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana wanaodaiwa ni Wamachinga wamemuua askari mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga na stuli kichwani wakati akitimiza majukumu yake. 
 
Marehemu Stephano Benjamin Komba (36) ambaye aliyekuwa na cheo cha sajenti.
Akizungumza na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa kuuaga mwili huo, Mkuu wa Oparesheni Manispaa ya Ilala, Charles Wambura alimtaja marehemu kwa jina la Stephano Benjamin Komba (36) aliyekuwa na cheo cha sajenti.
 
Mke wa marehemu Stephano Benjamin Komba (mwenye kilemba cheupe).
Alisema tukio hilo lilijiri Mei 16, mwaka huu, saa 7.30 mchana kwenye Mtaa wa Raha Kariakoo.
“Marehemu alikuwa na askari wengine walikamata baadhi ya bidhaa za Wamachinga kwa lengo la kuwaondoa lakini ghafla walivamiwa na kundi la wafanyabiashara hao ambapo Sajenti Komba akapigwa kichwani kwa stuli hali iliyomfanya apoteze fahamu kwa kuvuja damu nyingi.
“Askari walipambana na hao Wamachinga na kufanikiwa kumuokoa Sajenti Komba lakini akiwa na hali mbaya.
“Walimkimbiza Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo walimpeleka Muhimbili ambapo alifariki dunia saa 2:00 usiku,” alisema Wambura.
Mwili wa marehemu uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mbagala na kusafirishwa kwao Songea, mkoani Ruvuma kwa mazishi.
 
Mapadri wakiongoza ibada ya kumuaga marehemu Stephano Benjamin kwa safari yake ya mwisho.
Wambura aliongeza kuwa, hakufurahishwa na kitendo hicho cha Wamachinga kuchukua sheria mkononi.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutii sheria bila shuruti.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top