Suala la kukwama kufungwa kwa ndoa ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata limechukua sura mpya baada ya mzazi mwenza wa mchumba wa mbunge huyo, kukanusha taarifa kwamba alikwenda Dodoma kwa lengo la kuomba msaada kwa viongozi wa Bunge.
Kauli ya mama huyo imezidisha utata katika sakata la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo iliyokuwa ifanyike Jumamosi baada ya kutokea habari kuwa mwanamke mmoja alikwenda bungeni mjini Dodoma kutaka kuonana na Spika kwa lengo la kuomba Bunge limsaidie kupata haki yake kabla ya harusi hiyo kufungwa na hivyo kusababisha harusi kutofanyika.
Vicky Kamata, ambaye alijizolea umaarufu kutokana na wimbo wake wa “Wanawake na Maendeleo” na baadaye kuingia bungeni katika uchaguzi wa mwaka 2010, alikuwa afunge ndoa na mtu aitwaye Charles Gardiner Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam, lakini haikufanyika .
Jana, Kinavi Dadi, ambaye ni mzazi mwenza wa Gardiner, alikanusha kufunga safari hadi Dodoma kwa lengo hilo.
“Ni kweli kwamba Charles ni baba watoto wangu, lakini sijawahi kwenda Dodoma na wala sifahamu chochote kuhusu safari hiyo. Nadhani inatosha,” alisema mama huyo na hakutaka mazungumzo zaidi.
Baadaye kidogo mmoja wa ndugu wa Kinavi, ambaye aliomba asitajwe jina lake, alikiri ndugu yao kufunga ndoa na Gardiner Juni 2004 na kujaliwa kupata watoto wawili, lakini walitofautiana na baadaye ndoa yao kuvunjwa mwaka 2012.
Alisema taarifa kwamba aliyepata kuwa mke wa Gardiner alikwenda Dodoma kuomba msaada wa Bunge zimewaumiza sana kama familia kutokana na ukweli kwamba Kinavi ndiye anayefahamika kuwa mke wa kwanza.
Bungeni Dodoma
Wakati hayo yakiendelea, habari kutoka bungeni Dodoma zinasema mwanamke aliyedaiwa kuwa mke wa Gardiner ni‘feki’ na alikuwa wa kutengenezwa na baadhi ya wabunge kwa lengo la kumtibulia Vicky Kamata.
Mpango huo unadaiwa kuwahusisha wabunge wanawake wanne; watatu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chadema ambao awali waliapa kwamba ndoa ya mbunge mwenzao isingefungwa.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, waandishi wetu waliopo Dodoma walimsaka mwanamama huyo bila mafanikio na baadaye waliambiwa kwamba haikuwa rahisi kumwona kwani hakuwa halisi.
Kundi la wabunge hao ndilo lilimwingiza mwanamke huyo katika viwanja vya Bunge kwa lengo la kumkutanisha na viongozi wa taasisi hiyo, lakini mpango huo ulishindikana.
Mwishoni mwa wiki, Naibu Spika Job Ndugai alisema anakumbuka kwamba alipewa taarifa za kuwapo kwa mwanamke anayemtafuta, lakini hadi alipoondoka kwenda jimboni kwake Kongwa hakuwa ameonana naye.
Juzi Kamata aliliambia Mwananchi kwamba naye alisikia taarifa za kuwapo kwa mwanamke huyo mjini Dodoma, lakini hakuweza kufahamu ni nani kutokana na kwamba alikuwa bado amelazwa hospitalini.
Mbunge huyo alilazwa kwa siku sita katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea, Dar es Salaam na aliruhusiwa juzi. Anatarajia kwenda Dodoma wakati wowote.
Mapenzi ya Mungu
Mbunge huyo juzi alizungumzia kutofungwa kwa ndoa yake na kusema anaamini kilichotokea “ni mapenzi ya Mungu”.
Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam, Kamata alisema ingawa ndoa hiyo haijafungwa, moyo wake una amani kwa kuwa alimwomba Mungu kuhusu suala hilo kwa muda mrefu na hicho ndicho Mungu alichojibu.
Kamata alisema licha ya kuwa tukio la kutokufungwa kwa ndoa hiyo kuwa zito na ambalo lingeweza kumjeruhi moyo, amekuwa na amani tofauti na ndugu, jamaa na marafiki zake wengi walivyodhani.
Aliongeza kuwa anaamini kutokufungwa kwa ndoa yake kuna sababu ambazo Mungu mwenyewe anazijua na wala hawezi kumlaumu mtu au kulaani chochote kilichoingilia kati kufungwa kwa ndoa hiyo.
Kuhusu maandalizi ya harusi, alisema mipango mingi ilishafanyika na baadhi ya fedha zililipwa, lakini majadiliano yanafanyika kama waliokwishalipwa wanaweza kurudisha angalau nusu ya fedha.
Alisema baadhi ya fedha zilishalipwa kwa mpambaji, mpishi na mavazi ya harusi lakini ukumbi na vinywaji havikuwa vimelipiwa.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >