Habari Kali
Loading...

Majanga! Meno ya tembo yaibwa kituo cha polisi….

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== > Meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya vielelezo mahakamani yalitoweka katika Kituo cha Polisi cha Kilwa mkoani Lindi. Tukio hilo limenukuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikisema meno makubwa 108 ya tembo na kilo 20 za meno mengine ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa kama kielelezo cha kesi za uhujumu uchumi, yamebainika kutoweka kinyemela.
photo Polisi akilinda sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa Dar es Salaam hivi karibuni.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni juzi, imebainisha kuwa meno mengine makubwa ya tembo yaliyokuwa na uzito wa kilo 498.3 yamebadilishwa kinyemela na meno madogo, hivyo kusababisha hasara ya kilo 203.66 za meno ya tembo ambazo thamani yake haikufahamika.CAG Ludovick Utouh katika ripoti hiyo ya mwaka ulioishia Juni 30, 2013, amebainisha kuwa kumbukumbu katika Pori Tengefu la Miguruwe zilionyesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Juni 5 hadi Juni 8, 2012 meno makubwa 108 yalikuwa miongoni mwa vielelezo kituoni hapo.Kati ya meno hayo 108 yaliyokamatwa katika matukio ya ujangili, 74 yalitoweka katika kituo cha polisi wakati 34 yalibadilishwa na meno madogo, tofauti na yale yaliyokuwa yamekamatwa yakihusishwa na kesi ya ujangili Na. 3/2009 na kesi nyingine ya uhujumu uchumi Na. 2/2010 ambazo zilikuwa zikiendelea mahakamani mkoani Lindi.
Pia ilibainika kuwa kilo 20 za meno ya tembo ambayo yalikamatwa na kuhifadhiwa kama kielelezo cha majalada KLM/IR/184/2009, KLM/IR/235/2009 na KLM/IR/567/2010 yalitoweka.
Gari la ujangili latowekaUkaguzi huo pia ulibaini kuwa gari lililokamatwa likiwa kielelezo baada ya kukutwa na kilo 26 za meno ya tembo yenye thamani ya Sh135 milioni liliondolewa kinyemela katika Kituo cha Polisi Kilwa.CAG katika ukaguzi huo alibaini upungufu katika usimamizi wa meno ya tembo na nyara nyingine za taifa katika chumba cha meno hayo Dar es Salaam na vituo vya mikoani.CAG katika taarifa yake hiyo amesema kutokana na kukosekana kwa kumbukumbu sahihi, meno ya tembo yanaweza kuibwa au kupotea bila menejimenti kuwa na taarifa yoyote, hivyo ameishauri Serikali kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa kutosha katika usimamizi wa nyara za Serikali nchi nzima.
MWANANCHI

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top