Watu watano wasiofahamika wanaodhaniwa ni wezi, wamemvamia dereva wa lori la mafuta, Stephano John eneo la Kibamba, Barabara Kuu ya Dar es Salaam -Morogoro alipokuwa katika foleni na kisha kumpiga, kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili, kumfunga kamba na kumtupa mtaroni.
Ilielezwa kuwa baada ya kumfunga kamba, wahalifu hao walimdhibiti ndani ya lori na kutembea naye umbali wa kilomita moja walipofika maeneo ya Kiluvya ambako walimtupa katika mtaro na kuendelea na safari. Walifika mizani Kibaha wakapima uzito wa gari kama kawaida na kutokomea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea saa mbili usiku wakati dereva huyo akiwa kwenye foleni na lori lake aina ya Scania lililokuwa na tela pia lilikuwa na shehena ya petroli lita zaidi ya 39,000.
“Wakati dereva akiwa katika mwendo wa polepole kwenye foleni ya malori kuingia mizani, alivamiwa ghafla na watu watano waliofungua mlango na kuingia ndani.
“Wakati dereva akishangaa, walimnyanyua kwenye kiti na kumweka kiti cha nyuma na wakimtaka kukaa kimya,”alisema.
Kamanda Matei alimkariri dereva huyo akisema watu watatu walikaa kiti cha nyuma na mmoja kiti cha mbele na mwingine alikaa cha dereva na kuendesha lori hilo na yeye akiwa amewekwa chini ya ulinzi.
“Dereva alieleza kuwa alijitahidi kupambana nao ili achomoe ufunguo lakini, alizidiwa nguvu kwani walimkaba shingoni na alipojaribu tena kujinasua walimpiga sehemu za kichwani na kumfunga kamba. Walipofika eneo la Kiluvya walimshusha na kumsukumia mtaroni kisha wao kuendelea na safari. 
Akizungumza baadaye jana, Ofisa Habari wa Polisi Mkoa wa Pwani, Hassan Jumanne alisema katika msako uliofanyika juzi, lori hilo lilipatikana likiwa limetelekezwa eneo la Lugoba likiwa limeibwa mafuta yaliyokuwa katika tanki la tela.
Jumanne alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa lita za mafuta zilizoibwa ni 5,450 yenye thamani ya Sh11 milioni na kusema msako wa kuwatafuta waliohusika na tukio hilo unaendelea.
Awali, dereva Stephano alisema alikuwa akielekea Karatu na alifikwa na mkasa huo wakati utingo wake akiwa ametangulia mizani na kufanya ununuzi wa vyakula vya njiani ili kuokoa muda.
Hata hivyo, alisema utingo huyo alipoliona lori hilo mizani na kulifuata tayari kuendelea na safari, watu hao walimzuia.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >