Baadhi ya wamiliki wa Blogs nchini wakifuatilia mkutano huo.
Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia Andrew Kisaka akitoa mada katika mkutano na Bloggers leo.
Profesa
Nkoma (kushoto) pamoja na Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Aron
Msigwa (kulia) wakisikiliza maswali kutoka kwa wamiliki wa Blogs
(hawapo pichani).
WAMILIKI wa Blogs nchini wametakiwa kuzitumia vyema blog zao katika
kuripoti habari na matukio mbalimbali wakati wa uchaguzi wa serikali za
mitaa, wabunge na urais.Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma leo alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Blogs hizo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Profesa Nkoma alisisitiza kwamba wakati wa uchaguzi wamiliki wa Blogs wanatakiwa kutoa fursa sawa kwa kila upande pasipo upendeleo wowote wala uchochezi.
Aidha katika mkutao huo, wamiliki wa Blogs walikubaliana kuendeleza mchakato wa kuwa na umoja wao uliosajiliwa kisheria ambapo walichagua viongozi wa muda watakaosimamia mchakato huo.
Uongozi wa muda uliopitishwa na wamiliki hao ni kama ifuatavyo:
1.Joachim Mushi - Mwenyekiti
2. Francis Godwin - Makamu Mwenyekiti
3. Khadija Kalili - Katibu
4. Shamim Mwasha - Mjumbe
5. Othman Maulid - Mjumbe
6. William Malecela 'Lemutuz'- Mjumbe
7.Henry Mdimu - Mjumbe
TCRA imeahidi kutoa ushirikiano katika mchakato huo wa kusajili umoja wa wamiliki wa Blogs na kutoa elimu katika masuala mbalimbali yatakayosaidia jamii.
(Picha / Habari: Gabriel Ng’osha/GPL)
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

