HAIJAKAA sawasawa! Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine wakimtaka avue mataji mengine mawili.
Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.
Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss Tanzania zinaanzia vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa kwa hiyo kama skendo ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua kujisalimisha, basi bado hana sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji la Miss Tanzania kwa sababu ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu kudanganya umri bali ni kweli amedanganya, anajijua.
“Kama angekuwa hajadanganya, kwa nini asitoe paspoti yake inayomwonesha ana umri wa miaka 23? Mambo yalimfika shingoni ndiyo maana. Anachotakiwa ni kuvua taji la Miss Chang’ombe na Miss Temeke mwaka huu,” alisema Ismail Chandu, mkazi wa Temeke jijini Dar.
Shindano la Miss Temeke 2014 lilifanyika Agosti 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe jijini Dar ambapo Sitti Mtemvu aliibuka kidedea akifuatiwa na Salama Saleh (anayetakiwa kushika nafasi ya kwanza) na nafasi ya tatu ilitwaliwa na Neema Mollely.
Novemba 5, mwaka huu, Sitti Mtemvu aliiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake kuvua taji hilo.Sitti alifikia uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo ya kudanganya umri wakati akigombea taji hilo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

