MTOTO Happiness Lyoba (10)
ambaye aliripotiwa kuwa mwingi wa vituko vya maajabu, ikiwamo kuonekana
akishuka katika ndege huko Zanzibar, ameripotiwa kuokoka katika Kijiji
cha Mkokozi, wilayani Mkuranga, Pwani.
Akizungumza na gazeti hili, mama wa mtoto huyo, Salah Zefania alisema
mwanaye huyo alitoroka tena Septemba 16, mwaka huu na kukamatiwa eneo
la Feri jijini Dar es Salaam, akidai kuwa ameitwa na baba yake.
Baada ya kumkamata na kuanza kurejea naye
kijijini Mkokozi ambako amehifadhiwa na msamaria mwema, alisema alipata
simu nyingi za watu kumpa pole kwa tukio hilo, hali iliyomshangaza kwani
hakuelewa watu hao walipataje habari hizo.
Miongoni mwa simu hizo ni pamoja na ya
Mwinjilisti wa kanisa lao la Kisabato Mbagala aliyemtaja kwa jina la
Jacob Mayala ambaye alihitaji kumuombea mtoto wake. ‘’Ni kweli
Mwinjilisti huyo alifika Mkokozi na kufanya maombi maalumu
yaliyoambatana na kufunga kwa siku kadhaa. Hali ya mwanangu kwa sasa
ninakubaliana nayo maana amegeuka kuwa binadamu ambaye nilimtarajia,
Happiness hakuwa hivi maana alizidisha vituko vya maajabu,” alisema.
Mama huyo amewaomba Watanzania wamsaidie mwanaye kusoma kwani hivi
sasa anajitambua tofauti na huko nyuma.“Mimi kipato changu ni kidogo na
huku niliko ni mbali sana, hakuna shule karibu, kazi yangu ni kilimo cha
mbogamboga na tena hapa ninapoishi nimehifadhiwa tu, ninaomba msaada
ili mtoto wangu aende shule,” alisema mama huyo akidai kuwa Ustawi wa
Jamii ulimshauri kumweka binti yake mbali na maeneo aliyokuwa akiishi.
“Nilishauriwa asirudi Kitunda kwa muda huu
maana huko ndiko alikoanza kupatwa na hali ambayo naamini ilikuwa ni
mapepo,” alisema.
HAPPINES LYOBAKwa upande wake, Happines alisema anahitaji kusoma na kwamba matukio aliyokuwa akiyafanya hakujua yalivyotokea.
Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu ambaye akili yake imerejea kuwa ya kawaida kufuatia maombi ya kila siku, anaweza kuwasiliana na mama yake kwa namba 0768 632693.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

