Habari Kali
Loading...

HAUMUAMINI, UNAISHI NAYE KWA MACHALE, MAANA YAKE NINI? JIONGEZE!

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

NIMEFURAHI tumekutana tena katika safu yetu hii tunapata kujuzana masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.Ni mambo ya mahaba, hujakosea. Hapa tunaongeza maarifa ya mapenzi kila uchwao, karibu.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Natambua wengi tu wanaishi kwenye uhusiano wa namna hii.
Utakuta mtu anaishi kwa muda mrefu na mwenzake pasipo kuwa na imani naye. Anakuwa mguu ndani mguu nje kwamba yupo tayari kwa lolote, muda wowote.Eti anaamua kwamba bora penzi lake liende bila ya kuwa na malengo ya baadaye kwani hamuamini mpenzi wake.
Mtu wa aina hiyo mara nyingi anakuwa na hofu ya kupenda moja kwa moja kwa kuhofia kwamba asije akaambulia maumivu pale atakapozama moja kwa moja penzini.Unapokosa imani na mtu kwenye uhusiano ni hatari maana mapenzi yanajengwa na imani. Wapendanao lazima waaminiane, imani ikitoweka hakuna mapenzi.
Uaminifu unaanzia kwenye urafiki, uchumba na hata pale mtakapofikia katika hatua ya kuoana.
Imani inapopotea kwa marafiki, wachumba au wanandoa huwa kinachofuata penzi kusambaratika. Huwezi kuishi na mtu ndani ya nyumba ambaye haumuamini.Kukosa imani na mtu ambaye pengine unahitaji apite kwenye hatua za kuwa mchumba au kuwa mke na mume kuna madhara mengi lakini haya hapa chini ni baadhi:
KUTOFURAHIA PENZI
Imani inapokuwa haipo kwa mpenzi wako, kamwe hautoinjoi mapenzi. Utakuwa mtu wa hofu kila wakati badala ya kuipa nafasi furaha, kila wakati utawaza mambo mengi kwenye akili yako. Badala ya kufurahi faragha, wewe utawaza kusalitiwa.
Simu ikiingia katika simu ya mpenzi wako wewe tayari roho juu. Akili yako inakwenda mbali na kuhisi labda ni mchepuko wake. Wewe utakuwa ni mtu wa presha mwanzomwisho. Mapenzi matamu unakuwa unayasikia kwa wengine.
KUPOTEZA MUDA
Wakati unaishi kwa machale, muda nao siku zote huwa haumsubiri mtu. Miaka inaendelea kusonga huku wewe ukiendelea kudumu katika penzi ambalo halina mbele wala nyuma. Wakati wenzako wakifanya maamuzi sahihi ya kuingia kwenye ndoa wewe utakuwa unaishi kwa mashaka.
Kila siku utakuwa ukisogeza mbele uamuzi wa kuoana na mpenzi uliyenaye maana unaona muda bado wa kufanya maamuzi hayo, eti unasema ngoja umpe muda kidogo pengine kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, utamuamini. Kila siku unasema labda kesho kumbe miaka inazidi kukatika.
MALIPIZI
Umpendaye akigundua kwamba haumuamini, naye ataishi na wewe katika staili ya kutokuamini. Atakudanganya kama anakupenda kumbe moyoni naye hakupendi. Ni rahisi wakati huo na yeye kutumia nafasi hiyo kuanzisha uhusiano na mtu mwingine huku wewe akikufanya kama akiba.
Ataanzisha uhusiano na mtu ambaye anaamini kwamba naye anamuamini. Hatakubali kubaki na wewe peke yako huku akiamini kabisa humuamini na unaishi kwa machale.

Itaendelea wiki ijayo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top