NI SIMANZI! Msichana Yunis
Festo aliyekuwa na umri wa miaka 18 akisoma kidato cha nne katika Shule
ya Sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika Kijiji cha Bulima, wilaya ya
Busega mkoani Simiyu, alifariki dunia ghafla, saa takriban tatu tu kabla
ya kuanza mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari, alfajiri ya Jumatatu
wiki hii.
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili akiwa Busega, mmoja wa
walimu wa shule hiyo, Damian Kageba Lupimo alisema kabla ya umauti
kumfika, wiki moja nyuma alikuwa amelazwa katika zahanati iliyopo
kijijini hapo, hali iliyowalazimu wazazi wake kuja kumchukua na
kumpeleka Mwanza kwa matibabu zaidi.“Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell, lakini haikuwa siriaz sana, alirejea hapa shuleni Oktoba 31 mwaka huu.
Alihudhuria mahafali pamoja na wenzake Novemba Mosi na siku iliyofuata baba yake aliondoka kurudi nyumbani,” alisema mwalimu huyo na kuongeza kuwa usiku wake, akiwa bwenini na wenzake, hali yake ilianza kubadilika.
Alisema baada ya kuona mabadiliko hayo, wanafunzi wenzake walijumuika naye usiku huo wa saa tisa katika kufanya maombi, lakini saa moja baadaye, walilazimika kumkimbiza katika zahanati ya kijiji baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.
“Saa 11 alfajiri Yunis aliaga dunia na alisafirishwa siku hiyo hiyo kwenda nyumbani kwao katika kijiji cha Lijembe kilichopo Kwimba mkoani Mwanza ambako alizikwa Jumatano hii,” alisema mwalimu huyo.
Yunis Festo alizaliwa Februari 26, 1996 na kifo chake kimeleta simanzi kubwa kwa wanafunzi wenzake wa shule hiyo inayomilikiwa na Mchungaji Jofephares Mtebe yenye kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI. AMINA.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

