Habari Kali
Loading...

ZITTO KABWE ATWAA TUZO YA MTETEZI WA HAKI YA HIFADHI YA JAMII

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe (kulia), akizungumza na mmoja wa wakulima wa kahawa wilayani Kigoma Vijijini katika mojawapo ya ziara zake za kuhamasisha kilimo na kuhimiza wakulima kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe, ameibuka mwanasiasa wa kwanza barani Afrika kutwaa Tuzo ya Mtetezi wa Haki ya Hifadhi ya Jamii, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA)
Mhe. Zitto anatarajiwa kukabidhiwa tuzo yake hiyo katika sherehe rasmi iliyopangwa kufanyika Oktoba 30 na 31 mwaka huu katika mji wa Livingstone nchini Zambia.
“Tuzo hii imetolewa kwako kwa kuzingatia mchango wako mkubwa unaoutoa kuhakikisha sehemu kubwa ya Watanzania ambao walikuwa hawanufaiki na mifuko hii wanafaidika nayo.
“ECASSA, mahususi kabisa, imevutiwa sana na jitihada zako za kuhakikisha kwamba wasanii wananufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wakulima kupitia chama chao cha ushirika cha Rumako kilichopo Kigoma Vijijini,” ilisema sehemu ya barua ya umoja huo kwa Zitto
RUMAKO ni Ushirika wa Msingi wa Vijiji vya Mkabogo, Rusaba na Matyazo wilayani Kigoma Vijijini ambako zaidi ya wakulima wake 750 wameingia kuwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa takribani miaka minne sasa, Zitto amekuwa akipigania wakulima wa Tanzania kupewa uanachama wa wa mifuko hiyo ili kuwakwamua kiuchumi na pia kuwawezesha kupata huduma ya hifadhi kama ilivyo kwa wafanyakazi katika sekta rasmi wanaopata huduma hizo.
Baada ya wakulima hao wa Kigoma, kumekuwepo na wimbi la vyama vingi vya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini kutaka kuingia katika mifuko hiyo na ECASSA inaamini kwamba Zitto ana mchango mkubwa katika hilo.
Akizungumzia tuzo hiyo, Zitto alisema, " nimeipokea tuzo hii kwa unyenyekevu mkubwa. Naamini kuwa siku za usoni haki ya Hifadhi ya jamii kwa wananchi itakuwa ni haki ya kikatiba. Nchi masikini zinapaswa kuongeza uwekaji akiba ili ziweze kuendelea kwa kasi. Bila akiba uwekezaji unakuwa mdogo na hatimaye uchumi haukui.
"Hifadhi ya jamii ni moja ya njia mwafaka kabisa ya kukuza uwekaji akiba katika nchi kwani wanachama wanafaidika na mafao ya muda mrefu kama pensheni na yale ya muda mfupi kama Bima ya Afya na mikopo kupitia saccos".
Azimio la kutolewa kwa tuzo hiyo lilitokana na Mkutano Mkuu wa Sita wa ECASSA uliofanyika jijini Kampala, Uganda miaka miwili iliyopita, ambapo wakuu wa mifuko hiyo walikubaliana iwepo ili kuchochea wanasiasa kuhamasisha wananchi kuelewa umuhimu wa Hifadhi ya Jamii.
ECASSA ni umoja unaounganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii takribani 20 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zambia.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top