BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ni
jambo lisilofikirika kwa urahisi katika vichwa vya watu wengi lakini
mdadisi mmoja wa mambo juzi alinipa mtihani ambao nimebidi nijaribu
kuwashirikisha ninyi wadau wetu, maana baada ya mdadisi huyo kuuliza
swali mbele ya washkaji zake mimi nikiwemo, mjadala ukawa mkali sana
kiasi cha muafaka kutopatikana kwa urahisi.
Swali alilohusisha mdadisi huyo(jina kapuni) ni Je siku hizi wanawake natural wamepotea?
Mada
ilianza hivi baada ya hapo kila aina ya majibu yalitoka na muda
mwingine kuamsha taharuki, kila mtu akivutia katika pointi ama maoni
yake.
Baada
ya tafakari ndefu siku ya jana nikapata baadhi ya mambo ambayo naomba
wasomaji wetu tuchangie kadiri tuwezavyo. Katika tafakuri yangu nilianza
kuwachambua akina dada ambao tupo nao karibu.
Nikianza
na nilivyowajua baadhi yao wakati wakiwa bado vijana wadogo, nikagundua
kuna tofauti kubwa sana kati ya wakati ule na leo. Moja ya mabadiliko
ni pamoja na rangi na baadhi ya viungo katika ya miili yao.
Tofauti
hizo zinaanzia kichwani. Nywele zilizokuwapo kichwani mwao wakati ule
sio nywele za sasa. Sasa kuna ma weaving, Less wigs, Rasta za kusukia,
nywele za ki Brazilian na ki Hindi na kila aina ya vikorombwezo.
Ukishuka chini kidogo karibu na jicho nyusi za sasa nazo hazipo tena.
Sijui
sababu kubwa iliyopelekea jambo hili kutokea na badala yake mistari
yenye rangi ime replace nyusi za dada zetu. Usishangae kuona kope
nyekundu, blue ama rangi ya dhahabu.
Na
katika eneo hilo hilo kope za dada zetu siku hizi nazo zinachezewa na
kuongezewa mapambo. Ajabu na kweli.tukiwa bado tupo eneo hilo hilo la
kichwa tunashuka chini kidogo ni nadra kumkuta msichana siku hizi
ajapaka lipshine za aina mbali mbali ili kuongeza mvuto katika lips
zake.
Ukitoka
hapo unabaki na kichwa chenyewe hapo sasa ndipo uhalisia kwa asilimia
kubwa unapokuwa haupo. Rangi ya kichwa, shingo, na sehemu nyingine za
mwili kama mikono na miguu zinapishana kweli kweli. Siku hizi ni lazima
ujichubue ama uondokane na rangi yako uliyozaliwa nayo na uonekane na
muonekano wa Carolite ama vipodozi aina ya lotion.
Mtihani huo hata wanaume wamefeli pia siku hizi.
Ukiondokana
na eneo la kichwa unashuka kwenye fahari ya kwanza ya mwanamke ambayo
ni maziwa. Siku hizi wanasema kuna hadi Brazilia za kukuza matiti. Suala
hili limekuwa likiripotiwa katika magazeti ya udaku kwamba dada zetu
wanafanya kila aina ya jitihada alimradi wawe na maziwa makubwa. Sijui
maana yake ni nini hapo.
Ukitoka
eneo hilo unashuka kwenye fahari ya pili ya mwanamke hapo nazungumzia
hips na makalio. Sasa hapo pia hali imekuwa tofauti maana mchina ndiye
anyehusika sana nadhani kwa eneo hili sitaongelea sana kwani matokeo
yake yapo wazi na kwa sababu mjadala wa suala hilo umekuwa wazi sana.
Kikubwa
ambacho kinaonekana kwenye makala hii ni kwamba dada wa kike au
mwanamke wa leo anatawaliwa na vikorombwezo vingi ku boost image,
mwonekano ama mvuto wake kiasi kwamba ukikutana na dada zetu unashangaa
kimetokea nini. Hata kucha sasa kuna acrylic nails sasa hapo ana nini
cha kwake maana kila mahali ana modification?
Hapa
naomba nibalansi hii makala hatusemi kuwa mtu kupaka mafuta na kushine
ama kung’aa ni kuondokana na uhalisia. La hasha bali mwanamke wa leo
mathalani kuna sherehe basi tegemea kukutana vibweka. Mfano wa harusi,
ama kuna tukio la kijamii kama Miss Tanzania basi kazi kubwa katika siku
hiyo inafanyika saluni.
Na
huko ndipo gereji za kuondoa ama kubadilisha uhalisia wa dada zetu,
maana spea na spana zote za kufanyia kazi hiyo zipo huko. Mi ni kama
yule mdadisi ambaye anasema ame miss mwanamke natural wa kitanzania ya
na si photocopy ya Rihanna ama Nicki Minaj.
Naomba wewe mdau wetu na changie yako pia. Naomba kuwakilisha.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Monday, 27 October 2014