BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imesema haitawavumilia walimu walevi,
pia walimu wa kike wanaovaa mavazi mafupi na yanayoonesha maungo ya
miili yao na walimu wa kiume wanaovaa suruali za kubana ‘vimodo’. Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Ofisa Elimu wa Wilaya ya Bahi, Mary Mathew wakati
akizungumza na walimu wapya wa shule za msingi kwenye semina elekezi
inayohusu utendaji wa kazi zao.
Alisema
ualimu ni kazi inayohitaji nidhamu ya hali ya juu kutokana na walimu
kuwa walezi wa watoto wanaokuwa wanawafundisha, kwa hiyo ni vyema
wakavaa mavazi ya heshima kutokana na wao kuwa kioo cha jamii.
Alisema ni marufuku kwa walimu kuvaa nguo fupi na zile zinazoonesha maungo ya miili yao.
“Walimu
watakiwa kuonesha maadili mema kwani ni mabalozi kwa jamii
inayowazunguka pamoja na wanafunzi wanaowafundisha,” alisema .
Alisema hatarajii kuona walimu wanavaa nguo zinazodhalilisha taaluma hata kama wao wanazipenda.
“Hasa
ninyi kinadada na hata vijana mkinivalia vimodo, kwa kweli
sitowavumilia walimu ndani ya Wilaya hii ya Bahi kwani mnatakiwa
kuonyesha mfano kwa jamii na wanafunzi mnaowafundisha,’’ alisema.
Pia
aliwataka walimu hao kuzingatia miiko ya kazi kwa mujibu wa waraka na
sheria za serikali, ili kuleta ufanisi katika kuboresha elimu.
Alisema
walimu wengi wanapopata ajira wamekuwa wakijisahau kama wao ni
watumishi wa Serikali na kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na waraka na
maagizo ya kazi zao.
Naye, Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Bahi
Fredrick Kayombo amewashauri walimu hao kutumia fursa zao katika
kuanzisha miradi itakayowafanya wakopesheke kwenye taasisi za kifedha.
Pia aliwataka hao wanapokuwa kwenye vituo vyao vya kazi kujihadhari na matumizi ya muda wa kazi pindi wanapokuwa kazini.
“Kamwe hatutawavumilia walimu watakaobainika kutumia muda huo wa kazi kwa unywaji wa pombe,” alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bahi, Rachel Chuwa alisema
wilaya hiyo imepata walimu wapya zaidi ya 70 na utaratibu wa mafunzo
elezi kwa walimu wapya una lengo la kuwaondolea woga na hofu walimu ili
waweze kufanya kazi zao vizuri.
Alisema mwaka jana wilaya hiyo
ilishika nafasi ya tano kati ya saba kwa ufaulu mkoani Dodoma na
anatumaini walimu hao watasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu kutokana na
kuonesha ari ya kufanya kazi.
“Nitasikia amani kubwa kama mtaipandisha Bahi na kuwa nafasi ya juu,” alisema.
Pia
aliwataka walimu hao kutulia kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na
baadhi ya walimu kuanza kuomba uhamisho kwa kisingizio cha ndoa.
“Kila
kitu kina utaratibu wake kumbuka umeshaingia kwenye ndoa na Serikali
kwenye hilo tutaangalia ya kisheria na yale ya kimahusiano hata masuala
ya ugonjwa yataangaliwa lazima tuheshimu sheria, kanuni na utaratibu wa
kufanya kazi,” alisema.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Matukio
Thursday, 9 October 2014