Habari Kali
Loading...

SIMULIZI TAMU YA KHADIJA KOPA - 5

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

ILIPOSHIA
Iliishia pale Khadija aliposema kwamba tayari alimaliza kufanya mtihani wa darasa la saba na hivyo kuelekea nyumbani. Huko, akamkuta mama yake, ilikuwa ni furaha mno kwani mapenzi juu ya mama yake yalikuwa makubwa.
ENDELEA..
Malkia wa Mipasho Khadija Omary Kopa.
Naweza kusema kwamba zamani ilikuwa tofauti na sasa. Kitendo cha msichana kumaliza darasa la saba kilikuwa ni cha kipekee sana. Wasichana wengi waliishia njiani huku wengine hata kwenda shuleni hawakuwa wakiruhusiwa, kitendo cha mimi kumaliza darasa hilo kilinifariji sana.
Maisha ya mitaani yakaanza rasmi, kila siku nilikuwa na ndoto ya kuwa muimbaji kama Bi. Kidude lakini sikujua pa kuanzia. Sehemu kama Zanzibar ilikuwa ni tofauti na Dar es Salaam, mtu unaposimama na kusema kwamba unataka kuimba nyimbo za kidunia, jamii kama ilikuwa haikuelewi.
Kule Zanzibar watu tulikuwa tukilelewa kidini sana, hakukuwa na ujinga na hata mambo ya kuimbaimba nyimbo tofauti na Kaswida, utamaduni huo ulikuwa ukianzia Bara na watu kuupeleka kule.
Kwa kuwa nilikuwa na kipaji cha kuimba, nilitamani kuimba kama Bi. Kidude lakini kitu kilichokuwa kikiniumiza kichwa ni kwamba ningeanza vipi kuimba nyimbo kama hizo, na kama ningeamua kuingia huko, mama angeniruhusu? Na hata kama angeniruhusu, jamii ingenichukuliaje? Yalikuwa maswali ambayo sikuwa na majibu nayo.
Khadija Kopa akiwa na wanawe Stejini.
AFARIJIWA NA BIBI YAKE
Siku zikaendelea kukatika zaidi, moyo wangu bado ulikuwa na presha kubwa juu ya matokeo ya darasa la saba ambayo yalikuwa njiani kutangazwa. Sikuwa na furaha, ishu ya matokeo, hata kama ulikuwa umefanya vizuri na ulikuwa bado ungeendelea kuwa na wasiwasi tu.
“Ninaogopa matokeo bibi,” nilimwambia.
“Usijali, utafaulu tu.”
“Lakini ulikuwa mtihani mgumu.”
“Ila si ulisoma?”
“Ndiyo bibi.”
“Basi utafaulu tu mjukuu wangu, halafu tutakwenda bara kutembea,” aliniambia.
Maneno yake yakanitia nguvu upya, katika hili ningependa kusema kitu kimoja kwamba mzazi au mlezi unapomwambia mtoto wako maneno ya kumtia moyo pale anapoonekana kukata tamaa, hujazwa nguvu mpya juu ya jambo lile kama ilivyokuwa kwangu.
Kuanzia siku hiyo nikaanza kujipa moyo kwamba ningefaulu mtihani wangu wa darasa la saba. Sikuonekana kuwa na wasiwasi tena, nikajiona ningefaulu kwa kuwa nilifanya mtihani ule nikiwa nimesoma kila kitu.Kulikuwa na baadhi ya marafiki zangu hawakuwa wakiniombea mazuri, bado walikuwa na wivu nami, kisa tu sauti yangu ilionekana kuwa gumzo, maisha yangu ya kuwa mtaratibu na huku nikiwa na marafiki wengi wa kiume.
Familia ya Khadija Kopa ikipiga picha na wasanii wa Ze Comedi.
MATOKEO YABANDIKWA
Baada ya miezi kadhaa kukatika, nikasikia kwamba matokeo yalikuwa yametangazwa na kubandikwa shuleni. Japokuwa nilikuwa nikijiamini sana lakini kujiamini kule kote kukapungua, nikaanza kujiuliza ingekuwaje kama ningefeli?
   Wakati najiuliza maswali hayo yote ndivyo ambavyo moyo wangu ulivyokuwa ukikata tamaa juu ya kufanya vizuri.
Siku hiyo, sikutaka kwenda kutazama na kulikuwa na baadhi ya wanafunzi wachache mno waliokwenda kutazama matokeo yao, mimi niliendelea na shughuli zangu kama kawaida.
Nakumbuka siku hiyo nilikwenda madrasa kama kawaida. Huku tukiwa tunaendelea na masomo kuna rafiki yangu akanifuata na kuniambia kwamba nilikuwa nimefaulu mtihani na aliliona jina langu ubaoni.
“Unasemaje?” niliuliza huku nikionekana kuchanganyikiwa kwa furaha.
“Umefaulu mtihani,” aliniambia rafiki yule.
“Umejuaje?”
“Nimeliona jina lako.”
“Kweli?”“Haki ya Mungu tena,” aliapia.
Sikutaka kuendelea na masomo kwani nilijua fika kwamba hata kama ningeendelea kuwepo mahali hapo bado nisingeweza kusoma vizuri kutokana na shauku ya kutaka kuliona jina langu ubaoni, nikatoka na kuanza kukimbia kuelekea shuleni.
Japokuwa nilikuwa na mwili mkubwa huku watu wengi wakifikiri kwamba nilikuwa mvivu, kwenye kukimbia nilikuwa hodari sana, nilimshinda mpaka rafiki yangu yule aliyeniletea taarifa.
Tulipofika shuleni, watu walikuwepo wengi, walikuwa wamekuja kutazama matokeo yao na ya ndugu zao. Nikaanza kuelekea kulipokuwa na ubao, nikaanza kupenyapenya katikati ya watu na kufika mbele kabisa.
Nikaanza kulitafuta jina langu.
Japokuwa rafiki yangu yule aliniambia kwamba nilikuwa nimefaulu lakini moyo wangu ukaanza kuingia hofu kubwa kwa kuona kwamba inawezekana rafiki yangu yule alikuwa amenidanganya.
Nikafanikiwa kuliona jina langu, nilikuwa nimefaulu kwa alama nyingi sana. Nilibaki nikiwa na furaha tele, sikuamini kile nilichokuwa nikikiona.
ARUDI NYUMBANI KUMWAMBIA BIBI
Nilichokifanya ni kuondoka mahali hapo na kuelekea nyumbani. Nilikuwa na furaha mno na nilikuwa nikikimbia kumfuata bibi yangu na kumpa taarifa juu ya kufaulu kwangu mtihani.
Hata Juzuu nililokuwa nimelishika nililiona zito, nilitaka kubaki mimi kama mimi. Nilipofika nyumbani, bibi hakuwepo, nilikuwa na shauku ya kumwambia juu ya kufaulu kwangu.Kama katika kipindi kile kungekuwa na huduma ya simu, nahisi ningempigia na kumwambia aniambie alipo na mimi nimfuate.
Baada ya saa moja bibi akarudi, kwa furaha nikamfuata na kumkumbatia. Alipigwa na mshangao, nilivyompokea siku hiyo ilikuwa ni tofauti na siku nyingine, alijua kwamba kulikuwa na kitu.
“Kuna nini?” aliniuliza huku akionekana kutokuelewa chochote.
“Nimefaulu mtihani.”
“Unasemaje?”
“Nimefaulu mtihani bibi,” nilimwambia kwa furaha, bibi akaonekana kuwa na furaha zaidi yangu. Sasa nikamsubiria mama, naye nilitaka kumpa taarifa hiyo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top