Habari Kali
Loading...

SI KILA MCHINJAJI LAZIMA ALE SHINGO

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Jamani mbona makubwa madogo yana nafuu eti inahuu, nani kakuambia aihuu? mtakalia vimaneno vya kijinga wakati nyumba inateketea. Sipendi jamani mbona hivyo! Nani kawaroga hadi mnajitoa akili wakati mnazo. Leo nimekuja mahsusi kwa ajili ya kukuteteeni wanawake wenzangu. Lakiniii ninachowatetea kwenu kimekaa vipi?
Nimepata maswali mengi juu ya matatizo ndani ya uhusiano, bwana mmoja analalamika kutoswa na mpenzi wake ambaye alijichinjia mwenyewe na kuamini shingo anakula mwenyewe, lakini maskini kaambulia manyoya, kuku wote kala mwingine yeye kaambulia kuchinja tu.
Jamani ninaozungumza nao si watu wazima waliovuka miaka 18 mbona mnanitolea mimacho kuonesha bado hamjanielewa namaanisha nini. Jamani kuchinja kuku ni kuondoa usichana wa mwanamke kwani kisu kikishapita kuliwa ni halali na shingo ni ndoa.
Baba wa watu baada ya kujichinja aliamini kabisa yule msichana ndiye wa kufa na kuzikana, lakini wajanja wakamu onjesha utamu na kumuachia manyoya na kubakia akilalama. Si yeye, kina baba wengi huamini kumtoa mwanamke usichana wake, basi unakuwa umemaliza kila kitu. Jamani kuchinja ni sifa lakini ujuzi ndiyo kinga ya uhusiano wako.
Jamani si kila mchinjaji hula shingo wapo wanaochinjwa bila kula na mla shingo akawa mtu mwingine kabisa tofauti na mchinjaji. Lakini naamini wapo wanaume wanaamini akishamtoa mwanamke usichana basi ndiye lazima atakuwa mkewe. Lakini wanasahau kuna watu ndiyo mchezo wao kukata kichwa na kumuacha kuku aliwe na mwingine.
Jamani mapenzi ya mwanamke ambaye hajaolewa hayatokani na kukatwa kinywa bali mapenzi ya dhati. Wanawake wengine si waaminifu kwa asili hata ukimkata kichwa bado atapaparika na kwenda kuangukia kwa mtu mwingine kwa vile tu alikuwa na wewe kwa sababu ya kitu fulani.
Jamani si kila anayekuvulia nguo ya ndani ana mapenzi na wewe, wengi wapo kimasilahi.  Siku hizi kumkuta msichana na shingo yake (Bikra) ni adimu kama maji jangwani. Hivyo basi kuitoa kwa chipsi yai haoni shida kwa vile zama za ndoa kupata sifa kwa ajili ya kumkuta msichana hajamjua mwanaume wake wengi wanaona imepitwa na wakati.
Jamani si kwamba nawatetea wanawake wapoteze usichana wao la hasha, sisi enzi zetu msichana aliyeolewa bila bikra alikuwa hana thamani lakini siku hizi imebadilika watu hawaamini msichana leo kuolewa akiwa na bikra tofauti na zamani watu walikuwa wanashtuka kusikia msichana hana bikra.
Jamani watoto wetu muone fahari kuolewa na bikra zenu, usikubali kuitoa kwa ajili ya chipsi kuku. Unayempatia zawadi ya usichana wako ndiye awe mumeo. Jamani na ninyi wanaume kuchinja si dawa ya kula shingo bali kuwa mbunifu ili kuku wako atulie (soma mada ya wiki ya jana ina kila kitu inayosema
UBUNIFU HUONGEZA LADHA YA MAPENZI.)
 Lakini bado nasisitiza kuku aliyechinjwa na mwenzako bado ni halali kula shingo yake. Nina imani nimesomeka vizuri. Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top