Habari Kali
Loading...

Sakata la Mfanyabiashara Aliyejilipua kwa Risasi jijini Arusha Mazito yaibuka

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
SAKATA la Mkurugenzi wa Kampuni ya Kitalii ya DAGT, Timoth Mroki, kujiua kwa kujilipua kwa risasi, limeibua mambo mapya kutokana na kuelezwa kuwa wivu wa kimapenzi.
 
Habari zilizopatikana jijini Arusha, zinasema kuwa Mroki (36), alikuwa na vimada wawili ambao ni wake za watu na kuwa kabla ya kujilipua kwa risasi na kupoteza maisha, alitoa taarifa kwa wanawake hao (majina yanahifadhiwa).
 
Imeelezwa kuwa Mroki alikuwa akitoka na wanawake hao kila mmoja kwa muda wake, lakini baadaye siri hiyo ilianza kuvuja na hatimaye vimada kufahamiana, ikiwa ni pamoja na mkewe kuanza kupenyezewa taarifa hizo.
busi
 
Mroki, ambaye pia ni Meneja wa Operesheni na Masoko wa Kampuni ya Tanzania Bush Camp, alijiua kwa kujipiga risasi Oktoba 25, mwaka huu, saa 1:00, baada ya kubaini kuwa vimada wake hao wamefahamiana.
 
Habari kutoka kwa mtu wa karibu zimesema kuwa, vimada hao baada ya kufahamiana, walikutana na kufanya mazungumzo kisha kupiga picha pamoja na kumrushia kupitia simu ya mkononi.
 
Kugundulika kwa siri hiyo, kulizusha taharuki kwa Mroki, hivyo kusababisha kuyumba kwa uhusiano baina yake na vimada hao, akiwemo mmoja ambaye pia ni mshirika wake kibiashara.
 
“Hawa wanawake wana siri nzito kuhusiana na kifo hiki kwa sababu kabla ya kufanya uamuzi, aliwasiliana nao…kikubwa awali walikuwa hawafahamiani ila baadaye walikutana na kuungana kuwa kitu kimoja.
 
“Haifahamiki ni kwa vipi walijenga urafiki, ila watu wa karibu wanasema walijipanga kumkomoa ili afilisike kwa kuwa kila mmoja alikuwa na malengo yake,” alisema mtoa habari wetu.
 
Kuungana kwa wanawake hao kumlichanganya Mroki, ambaye tayari uhusiano wake nyumbani pia ulianza kuwa tete baada ya mkewe kuhisi kuna mambo yanafanyika kinyume cha utaratibu.
 
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa miongoni mwa wanawake hao, yupo aliyejenga uswahiba na mke wa marehemu huku uhusiano wa kimapenzi ukifichwa chini ya mwamvuli wa biashara.
 
Chanzo chetu kimesema kuwa, kutokana na ukaribu huo, familia hizo zimekuwa na kawaida ya kutembeleana, ikiwa ni pamoja na watoto kukaa kwa siku kadhaa nyumbani kwa kimada mmoja.
 
Imeelezwa kuwa kutokana na kugundulika kwa siri hiyo, Mroki alichukua uamuzi wa kujimaliza ili kukwepa aibu mbele ya familia.
 
“Kugonga gari si sababu ya Mroki kujiua, ni kutokana na kutingwa na mambo mengi kichwani, hasa baada ya siri ya kimapenzi kuanza kubainika,” aliongeza mmoja wa rafiki wa marehemu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema Mroki alijiua kwa kujipiga risasi kifuani kwa kutumia bastola aina ya KEL –TEC yenye namba HCB21.
 
Katika taarifa yake, Kamanda Sabas alisema kabla ya tukio hilo, Mroki alikuwa na gari nambaT222CMX, aina ya Isuzu Double Cabin, iliyokuwa ikitokea Mbauda kwenda katikati ya jiji.
 
Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa kutokana na msongamano wa magari, Mroki alitanua barabara kukwepa foleni huku akiwa katika mwendo kasi.
 
Alipofika maeneo ya Shams, aligongana na gari la mizigo, mali ya Kampuni ya Gupta, lenye namba T548 BRL.
 
Taarifa ilisema pamoja na kusababisha ajali hiyo, Mroki aliendelea na safari yake ndipo madereva wa bodaboda walipoamua kumfukuza na kumkamata eneo la kona ya Nairobi Ngarenaro.
 
Mroki aliporejea eneo la tukio na kuulizwa sababu za kusababisha ajali na kuendelea na safari, alitoa bastola na kufyatua risasi mbili hewani na ya tatu kumpiga kifuani.
    

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top