 |
| Ray C na Zamaradi |
Ray
anaonekana kupevuka kiakili na kifikra sana siku hizi ! kupitia mtandao
mmoja wa kijamii, star huyo wa muziki wa Bongoflava amewashauri wasanii
kuacahana na beef za kijinga badala yake waonyeshane upendo na
kuspotiana katika kazi.
Ray
C pia hakusita kumuomba msamaha Zamaradi Mketema ambaye walikwaruzana
miezi michache iliyopita, huku pia aiwasihi Wema Sepetu na Kajala
kuonyeshana upendo kama awali na kusahau tofauti zao
"Kiukweli
huwa naumia sana ninapoona mastaa tunatumia muda mwingi kulumbana na
kugombana kwa mambo ya kipuuzi sana,mastaa wenzetu wa Nigeria
wanatushinda kwa mambo mengi sana sababu wao wanashirikiana na
kusapotiana katika mambo mengi sana na hata ukisikia wamepishana basi
ujue ni kwa ajili ya biashara tu na si vinginevyo! nilichogundua mimi ni
kwamba kumekuwa na makundi mbalimbali mitandaoni yanayokuza mambo na
kusapoti wasanii kulumbana mara Team Simba mara Team Nyani! naongea
kutoka. Moyoni kuwa watanzania tunasifika kwa kuwa na amani na upendo!
sasa iweje tena tuishi maisha ya kuchukiana na ugomvi badala ya kuishi
kwa amani?
Najua
sisi wasanii tuna mashabiki wengi. na tunawapenda na nyie mnatupenda
kwahiyo mnatakiwa kutupatanisha tunapogombana na si kutushabikia coz
mnaposhabikia ugomvvi ndio mnapotufanya tupoteze muda kulumbana badala
ya kutumia huo muda kufanya kazi zetu za sanaa kwa bidii tutangaze nchi
yetu tunapoteza muda kulumbana,wenzetu wanaigeria wako mbali sana kwa
sababu wanasapotiana sana! wasanii tuache bifu za kijinga na tutumie
muda mchache tuliopewa na mola kufanya kazi zetu kwa bidii tutangaze
nchi yetu ili vizazi vijavyo virithi bidii zetu,na naomba sana mashabiki
wote msapoti mazuri tuyafanyayo"
Ray
C pia hakusita kumuomba msamaha aliyekuwa hasimu wake Zamaradi Mketema
ambaye walidaiwa kumgombea Ruge miezi michache iliyopita na kurushiana
maneno mitandaoni
"Love
u zama n sorry for everything keep doing wat u do best @zamaradimketema
n hey dogo langu @wemasepetu and my friend @new_kajala tusameheane na
tupendane na tupige kazi Africa watutambue bana!!!!!!"