BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Jamani habari zenu.
Leo
nimetoka kanisani nikamkuta mgeni nyumbani kwangu muda wa saa mbili
asubuhi.naanbiwa alifika tu nilipotoka ile kumi na mbili kasoro.si
mwingine bali ni bint ambaye nilisimamia ndoa yake mwaka jana mwezi wa
kumi na moja ana mtoto mmoja na umri wake ni 26yrs.
Nilimkuta kavinba macho kwelikweli kama alilia vile nikamuuliza kulikoni asubuh yote hii na kuvimba macho nini shida?
akaanza kunihadithia kama ifuatavyo;
Madam, namchukia A na sidhani kama nitampenda tena kwenye maisha yangu acha tuish tu kwa kuigiza mtoto apate malezi yetu.
nilipomaliza
chuo mwaka 2010 nilipata kazi hapohapo chuoni kama tutorial assistant
nikafanya mpaka 2012 baada ya mume wangu kuniambia nihamie arusha ili
tufanye taratibu za utambulisho na kufunga ndoa.
Nilikubali
na ndio makazi yangu yakawa huku baada ya ndoa na kila kitu 2013
nilianza kutafuta kazi na nikapata hapahapa Arusha ndipo nikaitwa kwenye
usaili juzi ambapo jumatano yaani tarehe8/10 natakiwa kwenda.
Nikamtaarifu
mume wangu ndipo alipokuja juu kama moto wa kifuu kuwa hakuna kufanya
kazi niende dukani nikafanye nae kazi ya kuuza nguo.
nikamwambia dukani siend nataka kufanya kazi.
Akadai
kuwa mume wake ni bahili sana kwani hamjali hamnunulii nguo hanunui
vitu muhimu vya ndani kama vyombo na vingine vya kupendezesha nyumba kwa
madai kuwa havina ulazima kwa sasa.
Akiomba
hela ya salon atapigwa mdomo wee unadhani mimi nachimba hela? kusuka tu
elfu 20 na kashfa nyinginezo. Hata akisema anaomba elfu mbili
anamwambia yanini? Nguo za mtoto hanunui anasema si lazima kwa sasa.
Pia
anasema alivyorudi Arusha alikua naye huko kwenye maduka yao kabla hata
hajafunga ndoa yaani wakiwa wachumba, alikua anauza hata milion kwa
siku atapewa elfu 5 akiambiwa ni nauli akisema naomba hata elfu 10 mama
kaniomba anamwambia maisha ya mamako yanakuhusu nini angalia ya kwetu.
Akiondoka
kila siku eti anaacha elfu 10 mezani ya chakula hapo hakuna mchele
mafuta sukari na vinginevyo akimwambia naomba hela nifanye shoping hata
ya wiki tu anamwambia hakuna hela hiyo kama ni mchele nusu nunua mafuta
ya 500 nunua.
Basi akawa anananiambia amechoka kutembea na vibobo vya mafuta kila siku mtaani.
Akanambia
pia amekua akilazimika kutoka kwa wanaume wenye pesa ili angalao aweze
kujikidhi mahitaj yake muhimu maana mumewe hamjali.
Mume wake ni kijana mtanashati tu hata ukimuina huwezi kuamini mpole na mstaarabu.
Ana kipato cha kawaida tu nyumba amepanga ila ana gari na vinauli vya kuendea china kuchukua mzigo.
Elimu yake ni standard 7 na mkewe ni chuo kikuu, sijui sasa ni uelewa ama vip wanatofautiana.
Jamani kanieleza mengi ila kwa maelezo hayo bila shaka mmeelewa, nashindwa hata nimshauri nini na vipi.
Jamani
nyie wanaume nyie kama hamna uwezo wa kuwahudumia wake zenu waacheni
watafute.we unambana mkeo wakat uwezo wa kumhudumia huna?
Matokeo yake mtaletewa na magonjwa ndani kutokana na wake zenu kuchepuka.
Yangu ni hayo tu ila kama hii ndoa ungekua ndo mshauri ungemshauri nini huyu binti?
Nipo nae hapa natafakari tu nini cha kumwambia.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Monday, 13 October 2014