Mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la
Mwanaheri anadaiwa kunaswa kwa msala wa utapeli na kupewa kashikashi la
aina yake baada ya ‘kutaitiwa’ na wanawake wenzake ambao ni
wajasiriamali akisemekana kukomba mali zenye gharama za Sh. milioni
mbili.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari
wetu lilijiri Mlimani City jijini Dar, mapema wiki hii, mishale ya saa
10:00 jioni ambapo Mwanaheri aliwekewa mtego na wanawake hao wanaofanyia
bishara zao Kariakoo.
Kwa mujibu wa wanawake hao, Mwanaheri alikuwa akiwasumbua kwa muda mrefu bila kurejesha pesa za mali walizompatia katika kikundi chao ambacho kinajishughulisha na kuuza bidhaa za Forever Living.
“Mwanaheri aliingizwa kwenye kikundi na mama yake mdogo (jina kapuni), tukamwamini na kumpatia mzigo wa Sh. milioni mbili.
Kikosi kilichomnasa tapeli Mwanaheri kikiwa kazini.
“Cha kushangaza Mwanaheri aliondoka na hakuonekana tena, kila
tukimpigia simu hapokei na mama yake mdogo akimpigia anamtukana ndiyo
maana tukampangia mpango wa kumkamata ambao umekamilika leo,” alisema
mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Zainabu.Kwa mujibu wa wanawake hao, Mwanaheri alikuwa akiwasumbua kwa muda mrefu bila kurejesha pesa za mali walizompatia katika kikundi chao ambacho kinajishughulisha na kuuza bidhaa za Forever Living.
“Mwanaheri aliingizwa kwenye kikundi na mama yake mdogo (jina kapuni), tukamwamini na kumpatia mzigo wa Sh. milioni mbili.
Mama huyo alidai kuwa baada ya kuona
wamekosa njia ya kumkamata waliamua kumtafuta mtu aliyejifanya kuwa ni
mteja na kumpa namba yake ambaye aliomba wakutane Mlimani City kwani
alikuwa akihitaji mzigo mkubwa.
Umati wa watu wawaliokuwa eneo la tukio wakimshuhudia tapeli huyo.
“Bila aibu sijui alikwenda kutapeli kwa nani tena akakubaliana na
mteja wakutane Mlimani City ndiyo tukajipanga na kuja kumkamata.“Alipopigiwa na mama aliyeahidiana naye akaja na mzigo lakini alipotuona akaanza kukimbia tena alikuwa na wenzake, tuliamua kumkimbiza na kumtia nguvuni,” alisema Zainabu.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, wanawake hao wakishirikiana na walinzi wa Mlimani City walimwingiza Mwanaheri kwenye gari na kumpeleka kumuhoji kisha kumpeleka polisi ili kumfungulia kesi ya madai.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

