Wiki iliyopita tulianza na mada yenye kichwa cha habari hapo juu ‘Mwanamke akioelewa kuna ulazima wa kutumia jina la ukoo wa mumewe?
Niliishia kwenye kipengele cha MAJINA KUFA kwamba ndicho wanawake wengi wanachohofia pale wanapotumia ya ukoo wa waume zao halafu wakatengana mbele ya safari.
LAKINI HILI NALO LIPO
Pia, kuna ushahidi wa kutosha kwamba, baadhi ya wanawake wamekuwa wakipenda kutumia majina ya ukoo wa waume zao kama kujenga heshima kwenye ndoa sanjari na kumpa heshima mume na yeye pia, hasa wale wanaotumia majina matatu, ya kwake mawili na la ukoo wa mumewe.
NI KWELI KUNA HESHIMA?
Kwa mwanamke ni zaidi sana. Heshima ya kuitwa kwa jina la ukoo wa mumewe kunamuongezea uzito wa hadhi katika jamii. Hakuna sababu ya kupinga kwani mifano ni mingi, tena wapo wanawake ni wasomi lakini kwenye ndoa usomi wao wanauweka pembeni na kushuka ili kujenga heshima.
Baadhi ya vitabu vitakatifu, vina kumbukumbu ya wanawake waliowataka wanaume wawaoe lakini kazi ya kujilisha na kujivalisha iwe kwao wenyewe (wanawake) ilimradi waitwe kwa majina ya waume zao.Wiki hii tunaendelea…
ATHARI ZAKE SASA
Uchunguzi unaonesha kuwa, athari ya mwanamke kutumia jina la ukoo wa mumewe liko kwa pande zote mbili. Maana kwamba, mume au mke mwenyewe.
ATHARI YA KWANZA
Endapo itatokea bahati mbaya ndoa ikavunjika, mwanamke hupata tabu kubadili jina mara anapokutana na mwanaume mwingine akafunga naye ndoa kama na yeye atapenda mkewe aitwe kwa jina la ukoo wake.
Athari ya pili ni pale mwanamke kama alikuwa na nyaraka mbalimbali zenye jina lake na la ukoo wa mumewe kuendelea kutumia jina hilo ambapo wakati mwingine, upande wa mumewe wanaweza kumchukulia kama kujikomba kama si kujipendekeza.
UFAFANUZI KIDOGO
Hapa ninamaanisha kwamba, mke alinunua gari, shamba au kiwanja na kwenye hati ya manunuzi alitumia jina lake na la ukoo wa mumewe, wakitengana (kwa bahati mbaya), wengi wamekuwa wazito kuendelea kutumia jina hilo. Hujikuta katika gharama nyingine ya kubadili jina, wakati mwingine mpaka kuapa mahakamani.
KWA MUME
Kwa upande wa mume, kama mke ametangana naye na anaendelea kutumia jina la ukoo wake, huathirika pale mwanamke huyo atakapoishi maisha yasiyo na maadili, kama uhuni na utapeli, mara nyingi jina hilo huchafuka wakati walishaachana.
KINACHOTAKIWA
Ni kweli kwa ndoa za miaka hii ni kazi sana mwanamke kukubali kulitumia jina la ukoo wa mumewe lakini muhimu kujiuliza kwanza, ni kwa nini tuwe na ndoa zenye maono ya kuvunjika siku yoyote huku tukijua tuliapa kuishi katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe?
Yeyote katika ndoa akilijua hilo, hakutakuwa na wasiwasi wa mwanamke kuhisi ufahari kulitumia jina la ukoo wa mume wake.Asanteni sana! Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine motomoto.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

