Habari za Siku ndugu,
Nina
imani wengi wenu mna hamu ya kupata uhalisia wa habari zilizoenea
mitaani kuhusu mwanafunzi kumzalisha mwalimu wake katika shule ya Nkasi
ambayo ndiyo kituo changu cha kazi.
Nitafafanua kwanza kuhusu walimu wa kike ninaofundisha nao then ntafafanua mazingira ya kuandikwa hiyo habari ilivokuwa.
Kwanza
shule ya sekondari ya Nkasi ipo wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa. Shule hii
ina kidato cha 1 hadi cha 6 ikiwa na tahasusi za HGK, HGL, PCM na PCM
(wasichana na wavulana). shule ina walimu 5 wa kike kama ifuatavyo:
Madam
Kasanga, huyu ni mama wa makamo amehamia mwezi uliopita kutoka
morogoro, ana watoto wakubwa na mme wake ni askari magereza.
Madam
Mwamini, huyu ni mdada mdogo tu, ana mtoto mdogo ananyonyesha ni mke
halali wa mtu na anaishi na mmewe, mme wake anafanya kaz LAPF.
Madam
David, huyu ni mdada tumeripoti nae mwaka huu. Hana mtoto ila ni mke
halali wa mtu, mmewe ni mwalimu anafundisha Sumbawanga manispaa.
Madam ipungu, huyu ni msichana hana mtoto ila mpaka sasa nina kadi yake anatarajia kufunga ndoa mwez wa 12.
Madam Balama, huyu pia ni mdada na hana mtoto.
Pili,
mazingira ya hiyo habari kuandikwa ni kutokana na taasisi inayoitwa
TMEP (Tanznia Men Equal Partinership) taasisi hii inajihusisha na elimu
ya kuwahusisha wanaume katika maswala ya afya ya uzazi na malezi.
Taasisi hii inafanya kazi kwenye mikoa 2 tu yaani Rukwa na Singida.
Tar
1/10/2014 taasisi hii ilitembelea shuleni kwetu kama wakala kuja
kukagua maendeleo, viongozi hao wakiwa wameambatana na mwandishi wa
habari (Siame) alimuuliza mkuu wa shule (Mr. Manga) je! kuna umuhimu wa
hii elimu kutolewa ? Mkuu katika kujibu swali hilo akamwambia kuna
umuhimu sana kwani siku za nyuma katika shule ya msingi kabwe iliyopo
katika mwambao wa ziwa mwalimu wa shule ya msingi alizalishwa na kijana
wa kidato cha pili hii yote ikiwa ni kwasababu ya kijana kukosa elimu ya
malezi. Lakini tangu elimu hii imeanza kutolewa tumeona mimba za ovyo
ovyo kwa vijana zimepungua pia ushiriki wa wanaume kwenye masuala ya
malezi ya watoto umeongezeka.
Sasa
tatizo la waandishi makanjanja akaripoti kama ndio tukio jipya na
limetokea Nkasi akiongeza na ubunifu wa maneno ili habari yake ishike
kurasa za mbele za vyombo vya habari.
Kimsingi hakuna ukweli wowote
na sisi tukiwa kama taasisi tunafikiria kuchukua hatua za kisheria kwa
kuharibiwa Taswira yetu katika jamii.
Ukweli ndio huo ndugu zangu.
Ahsanteni.
Mwl Mwaipaja. M. l (akabhofu!!!!)
Nkasi High School
P.o Box 119
Namanyere- Nkasi