Mtaro
alijikuta juzi katika wakati mgumu baada ya wananchi wanaodai ni wenye
hasira kutaka kumpa kipigo kwa kitendo hicho cha kugeuza sehemu ya
makaburi kuwa eneo la burudani.
Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mfanyakazi Idara ya Fedha ya
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, inadaiwa alianzisha biashara hiyo ya
vileo katika eneo la Roben Kata ya Mkuti, mjini Masasi wiki mbili
zilizopita.
Tafrani
iliyojitokeza juzi na kudumu kwa zaidi ya saa saba, ilikuwa ni baada ya
kundi la vijana kufika eneo hilo kwa ajili ya kuchimba kaburi kwa
maziko ya ndugu yao na kukuta hali tofauti.
MKAZI
wa Mtaa wa Misufini, Kata ya Nyasa, Halmashauri ya Mji Masasi mkoani
Mtwara, Innocent Mtaro anatuhumiwa kujenga baa katikati ya makaburi.
Inadaiwa
walikuta baadhi ya makaburi yamejengwa sehemu za kukaa wateja, choo
pamoja na banda kubwa la biashara lililosheheni vinywaji. Aidha
walikasirishwa na kile kinachodaiwa kwamba ni kukuta pakiti tupu za
pombe zikiwa zimetapakaa juu ya makaburi hayo.
Inadaiwa
pia walikutwa wateja wakipata vinywaji wakati huo saa 4 asubuhi huku
baadhi wakiwa wameweka miguu juu ya makaburi; kitendo kilichoibua hasira
ya vijana hao walioamua kutoa taarifa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mkuti.
Mmiliki
Akizungumza
kwa niaba ya mmiliki, Meneja wa ‘baa’ hiyo, Gasper Priscus alisema
waliamua kujenga kwenye eneo hilo kwa kuwa kiwanja hicho wanakimiliki.
Alidai
waliuziwa na mkazi wa Kitongoji cha Roben mjini Masasi, Gerald Daudi.
Kwa mujibu wa meneja huyo, baada ya kuuziwa waliamua kuanza ujenzi wa
baa hiyo kwa haraka kwa madai kuwa aliyewauzia, Daudi ni mgonjwa.
Priscus
alisema walikuwa na hofu kwamba endapo angefariki kabla ya kujenga baa
hiyo, wangenyang’anywa eneo hilo kwa kuwa limeshazungukwa na makaburi.
Alikiri
kwamba takribani wiki mbili sasa zimepita tangu waanze biashara hiyo ya
vileo kwenye eneo hilo na kwamba wamekuwa wakipata wateja wengi hasa
usiku.
Akana kuuza
Hata
hivyo Daudi; anayedaiwa kuuza eneo hilo kwa Mtaro alikana kuliuza.
Alisema aliamua kumpa eneo hilo bure kwa jinsi anavyomsaidia katika hali
yake ya ugonjwa ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.
Akizunngumzia
kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya misalaba kupisha ujenzi huo, Daudi
aliyekuwa akizungumza kwa taabu akiwa kitandani, alisema walikubaliana
ing’olewe mitatu pekee kutoka kwenye makaburi ya familia yao.
Alisema uamuzi wa kung’oa misalaba mingine zaidi ya 10 ni uamuzi uliofanywa na aliyemkabidhi eneo hilo.
Ofisa
Mtendaji Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuti, Moza Napachili alithibitisha
ofisi yake kupokea taarifa za kuwepo kwa mtu aliyejenga baa kwenye eneo
la makaburi.
Napachili alisema alikwenda kwenye eneo la tukio akiongozana na Mwenyekiti wa mtaa huo kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Baadaye
kilifanyika kikao baina ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Masasi, Henry Kagogoro, Mtendaji wa Kata, wa Mtaa, na Mwenyekiti wa
Halmashauri pamoja na anayedaiwa kuwa mmiliki wa baa hiyo, Mtaro.
Makubaliano
yaliyofikiwa na kikao hicho ni kutaifisha eneo hilo. Walikubaliana
libaki chini ya Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maziko pekee.
Hivyo
iliamuriwa jengo hilo la baa na vibanda, viondolewe na mhusika, kesho
awasilishe taarifa Idara ya Ardhi zinazoonesha kuwa eneo hilo
analimiliki kihalali. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri alisisitiza eneo
hilo la makaburi ni mali ya Halmashauri.
Wateketeza kwa moto
Hata
hivyo wananchi waliokuwa wamefika kwenye makaburi hayo kwa ajili ya
kuzika ndugu yao, waliteketeza kwa moto vibanda vitano vya kupumzikia
vilivyoezekwa kwa makuti. Pia jengo la baa lilibomolewa.
Polisi
Kwa
upande wa Polisi, ilikiri kuwa na taarifa juu ya mgogoro huo. Mkuu wa
Polisi, Wilaya, Azaria Makubi alisema wanaendelea na upelelezi kuhusu
tukio hilo.
-mpekuzi