Habari Kali
Loading...

MSANII AIBUA TIMBWILI KANISANI!

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Mauzauza? Katika hali ya kushangaza, mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry anadaiwa kuzua timbwili kanisani na kusababisha tafrani madhabauni ikisemekana ni mapepo.
Mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry akiwa katika hali ya sintofahamu.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patriki mjini hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati wa kuaga mwili wa msanii mwenzake, Shirley Edward almaarufu Sherry Magali.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakichukua uamuzi wa kumtoa nje ya kanisa ili ibada ya mazishi iendelee.
Awali, kabla ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu, Jasmini, akiwa benchi la mwisho nyuma sambamba na wasanii wenzake akiwemo Asha Boko na mke wa Mzee Majuto, Rehema Majuto, alionekana mwenye simanzi kupita kiasi.
Msanii Jasmini Emiry akibebwa kuelekea nje ya kanisa.
Ulipofika muda wa kuaga, Jasmini alipomaliza kulizunguka jeneza lililobeba mwili wa Sherry mbele ya madhabahu, alianguka na kuanza kurusha mateke kama punda huku akizungumza maneno yasiyoeleweka.
Jasmini Emiry akiwa amelala mbelea ya gari alilotaka limkanyage.
Baada ya kuona hivyo, baadhi ya wasanii wa Bongo Movies mjini hapa wakiongozwa na Chediel Senzighe walimbeba msanii huyo na kumtoa nje huku akiwapiga na kuzua tafrani ya aina yake.
Waombolezaji wakiendelea na shughuli za mazishi baada ya tafrani hiyo.
Alipofikishwa nje, Jasmini alilala kwenye tairi la gari Toyota Coaster akitaka limkanyage afe na alipotoka hapo alikimbilia ofisini kwa paroko na kujilaza kwenye kiti ambapo wasanii wenzake walimkamata na kuondoka naye kwenye Coaster kisha kwenda kuzika Makaburi ya Kola mjini hapa.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top