WIVU wa mapenzi bwana! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la David Patrick Chagu (pichani) aliyekuwa akiishi Jimbo la George nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ amekumbwa na mauti kwa kuchomwa visu na mpenziwe aliyefahamika kwa jina moja la Monica.
Kwa mujibu wa chanzo, marehemu alichomwa
visu na mpenzi wake huyo ambaye ni Mzungu kwa madai ya wivu kufuatia
kutomwona kwa siku tatu na kumhisi ana mpenzi mwingine.
Akizungumza na Uwazi kwa majonzi makubwa,
mama mzazi wa marehemu, Rose Ndunguru ambaye ni Katibu wa Umoja wa
Wanawake wa CCM Kata ya Ubungo alisema alipatwa na simanzi kubwa
kutokana na kitendo hicho alichokifanya mkwewe ambaye alikuwa akimpenda
mno na kutoamini alichomtendea mwanaye.
“Naumia sana jamani sijui nielezeje! Chanzo
cha yote Monica alinipigia simu akasema ana siku tatu hajaonana na
David kwa kuwa walikuwa hawaishi wote.“Alisema nimpigie simu David,
nimwambie mtoto anaumwa, ndipo mwanangu akaenda na kumkuta mtoto mzima
isipokuwa alikuwa akisumbuliwa na mafua.”
“Siku iliyofuata, kwa kuwa David ni
mfanyabiashara mbali ya kuwa ni mwanafunzi katika Chuo cha Wescaptown,
akiwa anatoka kwenye biashara zake alikwenda nyumbani kwa Monica
kumrudisha shemeji yake wa kiume akiwa na gari.
“Aliposhuka tu akiwa eneo la wazi la
barabara ndipo Monica akamchoma visu vitatu, kifuani na cha mkononi bila
huruma,”alisema mama huyo.Aliongeza kuwa, kutokana na tukio hilo
ambalo lilitokea usiku wa Alhamisi mwanaye alikimbizwa kwenye Hospitali
ya Mozaribay iliyopo palepale George, lakini baada ya nusu saa akafariki
dunia.
“Monica alikamatwa asubuhi yake na kuwekwa ndani japo mpaka sasa yupo nje kwa dhamana.“Inasikitisha sana kwani sasa amekuwa akinisumbua kwenye simu akitaka matumizi ya mtoto na kuniambia nimsamehe kwa alichofanya kwani hakukusudia.”Mama huyo alisema yeye ameshamsamehe Monica kwa yote yaliyotokea na kumwachia Mungu.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

