BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,
Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia
yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara
ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko
tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna
sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni
kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume).
Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially
akina mama.
Hivi
karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe
japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi
kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa
mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia.
Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa
Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza
kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole
tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).
Baada
ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende
kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo.
Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku
mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua
alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.
Baada
ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4,
ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje
maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie
tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.
Siku
moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia.
Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo
baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa
sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji
kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo
na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata
simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na
hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao,
japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.
Najua
fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote
yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake.
Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa
visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment
zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi
kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na
kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu
chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa
wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi
sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini
mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Thursday, 30 October 2014