KWAKO Miss Tanzania usiyechuja tangu mwaka 2006 hadi leo? Hongera kwa ‘ku-maintain’ ustaa wako tangu miaka hiyo hadi leo.
Ni
matumaini yangu u-mzima wa afya. Ukitaka kujua afya yangu, namshukuru
Mungu niko poa, naendelea kulisogeza gurudumu la maendeleo kupitia
kalamu yangu.Madhumuni ya kukuandikia barua hii si tu kukujulia hali,
bali pia kukukumbusha juu ya maisha yako ya kistaa.
Eee, we ni staa kwelikweli nani asiyekujua!
Kwa
kipindi cha hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia juu ya mbwembwe zako na
jeuri ya fedha. Ulianzia kwenye Bendi ya Skylight ukafanya kufuru,
baadaye mtoto wa kike ukasababisha tena kwa Yamoto Band, kijana Aslay
atakuwa kakushukuru kweli kwa mvua ya fedha uliyomwagia.
Yawezekana
upo katika ‘kaligi’ ka upinzani na aliyekuwa shosti wako, Kajala
Masanja ambaye naye alionesha mbwembwe za namna hiyo hivi karibuni
lakini pointi ya msingi hapo ya kujiuliza, zipo nyingi kiasi cha
kuzimwaga?
Kila mtu anatambua kwamba fedha zinazotoka bila kuingia mwisho wake ni nini? Zitaisha.
Nakumbuka
kabla haujaendesha kaligi ulikoibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya
mpinzani wako Kajala, ulikuwa kimya kuonesha zilikuwa zimeanza kukata.
Sasa naona zimekutembelea kwa mara nyingine, jeuri imerudi palepale. Unamwaga fedha ili zikuzoee? Mh! Sidhani kama ni sawasawa.
Japo
sina uhakika sana uwepo wa miradi yako, lakini nafikiri ukianzisha
miradi kupitia fedha unazozimwaga kwa sasa zinaweza kukusaidia huko
mbeleni. Starehe zipo lakini ‘kuzi-controo’ ni muhimu.
Hata
katika eneo lako la kazi, mashabiki wako wamekuwa wakilalamika sana
hawapati kazi mpya kutoka kwako. Kupitia fedha hizo, unaweza pia
kuimarisha kampuni ya kuzalisha filamu na ukatoa filamu za kukidhi
mahitaji ya mashabiki wako lukuki walioko nchi nzima.
Una
bahati ya kupendwa, una wafuasi wengi wanaokufuata kwa nini usiitumie
vizuri nafasi hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama kipindi kile
ulichokuja moto na kipindi cha In My Shoes? Hivi kiliishiaga wapi kile
kipindi? Nini kilitokea?
Ninachopenda kuona kutoka kwako ni wewe kuzitumia fedha kwelikweli lakini pia ziingie kwelikweli, zaidi ya zile zinazotoka.
Kama ni muelewa, elewa na yafanyie kazi mawazo yangu. All the best!