BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Moshi.
Mgogoro mwingine mkubwa wa kifamilia wa kugombea maiti, umeibuka mjini
Moshi na kusababisha mwili wa Rosemary Marandu (38), kuhifadhiwa
mochwari kwa siku 34.
Mwili
wa marehemu huyo aliyefariki dunia Septemba 4, mwaka huu umehifadhiwa
katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na umekuwa ukilipiwa Sh9,000 kwa siku,
hivyo siku 34 gharama yake imefikia Sh306,000.
Tukio
hilo limekuwa gumzo mjini Moshi hasa baada ya kutokea siku chache baada
ya maiti nyingine ya Steven Assey kufukuliwa kwa amri ya Mahakama na
hadi leo ni siku ya 29 bado haijazikwa licha ya mke mdogo wa marehemu,
Fortunata Lyimo kupewa haki ya kuzika lakini amekataa akisema ni kinyume
cha mila na utamaduni wao kwa mtu kuzikwa mara mbili. Akizungumza jana,
mama mzazi wa Rosemary Marandu, Felicia Nkya, alidai kuwa mumewe
aitwaye Flavian Marandu ndiye anayeshikilia mwili huo hadi leo.
Marandu
ni Diwani wa Kata ya Mrao Keryo kwa tiketi ya CCM na anamiliki vitega
uchumi kadhaa vikiwamo viwanda vya kupasua mbao na nyumba za kulala
wageni.
“Ukweli
ni kwamba tangu amekufa (Marandu) hajatupa taarifa yoyote zaidi ya
kunitumia meseji ya simu akiniuliza kama mume wa Rosemary ameniambia
kama Rosemary amekufa. Kwa mila na utamaduni wetu, mtu akifa tunakaa
pamoja na kupanga mazishi lakini hadi leo hajatuma mtu yeyote kuzungumza
na sisi juu ya msiba.”
Felicia
alisema walitengana na mumewe huyo mwaka 1982 na mtoto wao huyo amezaa
watoto wanane na wanaume tofautitofauti na mumewe aliyemfia, Sigfrid
Mlingi naye amezuiwa kumzika.
“Naumia
sana napata mateso makubwa ya kiakili na kisaikolojia. Mwezi mzima sasa
sijui hatima ya mazishi ya mtoto wangu. Hakuna chakula kinachopita
naomba mnisaidie jamani,” alilalamika.
Mama
huyo alidai kuwa awali walikwenda kulalamika polisi ambako walishauriwa
kufungua shauri mahakamani lakini akadai kwamba hawana nguvu ya
kushindana na Marandu.
“Tumeamua
kumkabidhi Mungu kwa sababu hatuwezi kushindana naye (Marandu)
tukamshinda. Hata kule KCMC anadai kuna kesi mahakamani lakini sisi
hatujafungua kesi,” alidai.
Mlingi alisema ameamua kujiweka kando kushughulikia mazishi ya mkewe baada ya baba mkwe kumtolea lugha isiyofaa.
“Mimi
ndiye nilimuuguza hapo Mawenzi mpaka akanifia mikononi mwangu na baada
ya kufa nilikwenda Keryo na kuonana na baba yake lakini akanifukuza,”
alidai Mlingi.
Alisema
awali walikubaliana kufanya maziko Septemba 9, mwaka huu katika
Makaburi ya Karanga, Moshi lakini baadaye baba yake akabadilika na
kukataa.
“Aliwapigia
simu ndugu zangu na kuwatolea lugha isiyofaa na mimi mwenyewe
akanitolea kauli za kunidhalilisha na baada ya hapo nikanawa mikono,”
alidai Mlingi.
Baada
ya kushindwa kuelewana, Mlingi alidai Marandu alituma watu wawili
katika Hospitali ya Mawenzi ambao waliouhamisha mwili wa mkewe na
kuupeleka kuuhifadhi KCMC.
Alisema hajui kama mkewe ambaye amezaa naye watoto watatu alishazikwa au la na kwamba kwa yote yaliyotokea amemwachia Mungu.
Baba aeleza sababu za kutozika
Hata
hivyo, akizungumza kwa simu kutoka Iringa, Marandu alikanusha kuwa
kiini cha kutozikwa kwa mtoto wake huyo akisema anasita kuzika bila
kupata ridhaa ya mama yake.
“Hao
(mama na mume) wananizushia maneno mengi sana, lakini ukweli ni kwamba
tangu amekufa hawajataka kuja tuzungumze pamoja na kupanga mazishi”
alidai Marandu.
Marandu
alidai kuwa mzazi mwenzake huyo alikwenda mbali na kumshtaki polisi
ambako rafiki yake wa karibu ambaye ndiye aliyekwenda kuuhifadhi mwili
KCMC kwa niaba yake, alikamatwa na kuhojiwa.
“Hivi
leo katika mazingira hayo nikizika halafu akatokea mume wake
akanishtaki akidai haki ya kuzika si maiti itafukuliwa? Ndiyo maana
nataka waje tukae tuzungumze tupange mazishi pamoja”.
Marandu
alisema ili kuepusha kadhia, ameona ni busara utata huo ukatatuliwa
kwanza na njia pekee ni pande zote zinazohusika kushiriki katika kupanga
mazishi hayo.
Lakini
badala yake, Marandu alidai kuwa mama wa marehemu anashirikiana na
baadhi ya ndugu kutoa matangazo ya uongo redioni kuwa mazishi yamepangwa
kufanyika keshokutwa wilayani Rombo.
“Mimi
sijawahi kutoa tangazo redioni linalohusu mazishi lakini ni wao
wamekwenda redioni na kutoa tangazo hilo,” alidai Marandu na kusema
atarejea Moshi kesho kushughulikia suala hilo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Matukio
Saturday, 11 October 2014