WANAFUNZI wawili wa shule za msingi za Nyabisara (Murito) na Kerende Kata ya Kemambo wilayani Tarime, Mara wameumwa hadi kuondolewa nyama zao za miguu na mamba walipokwenda kuoga maji ya mto kwa nyakatitofauti.
Wanafunzi hao ni Penina Joseph Mangure (11) wa darasa la nne Shule ya Msingi Nyabisara katika Kijiji cha Murito ambaye ni mtoto wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Joseph Mangure na Stephano Stephano (11) pia wa darasa la nne Shule ya Msingi Kerende.
Taarifa za madenti hao kukutwa na mkasa huo zilifikishwa katika Kituo cha Polisi Nyangoto (Nyamongo) na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, baba wa Penina alisema mwanaye aliokolewa na wananchi baada ya kupiga kelele wakati akiwa ameshikilia nyasi zilizomsaidia kushindwa kutumbukizwa majini na mamba huyo ambaye alikwenda na kipande cha nyama ya mguu wa kushoto.
Kwa upande wake mtoto Stephano alidaiwa kukutwa na tukio hilo alipokuwa akioga maji ya mto huo wakati akichunga ng’ombe wa nyumbani kwao.Mtoto huyo alifanikiwa kuokolewa na wasamaria wema alipokamatwa na mamba huyo baada ya kupiga kelele na kufanikiwa kumtoa mguu katika mdomo wa mamba lakini akiwa ameshamnyofoa kipande cha nyama mguu wa kushoto pia.
Mwenyekiti huyo alisema tangu Januari hadi Oktoba mwaka huu, watu watano wa kijiji chake wameshapoteza maisha baada ya kuliwa na mamba kwa nyakati tofauti huku wengine takribani 100 wakijeruhiwa.
Pia mwenyekiti huyo alisema mto huo kupita katika makazi ya watu ni tatizo na kwamba kila mara wananchi wanapopatwa na adha hizo huwasilisha taarifa katika Halmashauri ya Wilayani Tarime kupitia kitengo cha wanyama pori kwa ajili ya kusubiri hatua zaidi.
Alimuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu kuhakikisha inawafidia wote waliojeruhiwa au kupotozewa maisha na mamba hao.Watoto hao bado wanasota majumbani mwao baada ya tiba ya awali huku wazazi wao wakitafuta fedha ili wapelekwe Hospitali ya Bugando, Mwanza kwa matibabu zaidi.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

