Habari Kali
Loading...

LINEX: NISINGEKUWA MWANAMUZIKI NINGEKUWA ASKARI

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Makala: SHANI RAMADHANI
MWANAMUZIKI mahiri wa muziki w Bongo Fleva nchini, Sande Mangu ‘Linex’ au ‘Voa’ amesema kabila lake linamsababisha kupata ‘tone’ ambayo mtu mwingine hana na kuna baadhi ya wasanii ambao wanatamani wawe wanajua lugha za kwao.
Host wa kipindi cha Mtu Kati cha Global TV Online, Pamela Daffa (kushoto) akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva, Linex (kulia).
Akihojiwa na safu hii, huku akirekodiwa na ‘kruu’ ya Global Tv Online mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chumba cha Habari cha Global Publishers, Linex alisema asingekuwa mwanamuziki angekuwa askari, ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia unaweza kuyapata  kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com .
Mwandishi: Huwa unajiita Voa, ni nini maana yake?
Linex: Dah aisee Voa kirefu chake ni Voice of Africa yaani maana yake ni Sauti ya Afrika niliamua kujiita hivyo kwa jinsi sauti yangu ilivyo na ninavyoimba.
Mwandishi: Wewe ni kiongozi  wa Kundi la Kigoma All Stars?
Linex:  Kigoma All Stars ni vijana kumi na kadhaa ambao ni maarufu na wanaotokea sehemu (mji mmoja) walikutana mjini wakaamua kushirikiana na kufanya kitu cha pamoja ambacho siyo lazima kifanyike tena.
Linex akifafanua jambo wakati wa mahojiano.
Mwandishi: Ilikuwaje mpaka mkaamua kufanya kitu kama kile, je huwa mnapeana sapoti katika kazi zenu?
Linex: Ni jinsi ambavyo binadamu tunaishi siyo kwamba watu tumefanya wimbo wa pamoja ndiyo tukawa tunasapotiana ile ni kazi na tulikutana kazini na kwenye maisha ya kawaida kila mtu anaweza kuwa na maisha yake.
Mwandishi: Una ukaribu gani na Mhe. Zitto?
Linex: Mh. Zitto naishi naye freshi yaani kama braza mtu ambaye anapenda sanaa zaidi kile ambacho ninakifanya na tumejuana kimjinimjini.
Mwandishi: Ulishawahi kuwaga na mpenzi Mzungu, hatukuoni naye na wala hatusikii chochote vipi?
Linex: Sasa hivi ninapenda maisha yangu  yawe siri siyo lazima kila ninachokifanya mtu ajue kwa sababu nimetokea kwenye maisha fulani ya kushindwa kumudu hata tumbo langu mwenyewe na hata nauli ya daladala, Mzungu alikuwepo juzi tu hapa Bongo kakaa kama mwezi hivi kaondoka.
Mwandishi: Vipi kuna usumbufu wowote unoupata kutoka kwa wadada wa mjini?
Linex:  Aaah! Mi sipati usumbufu wowote labda kwa sababu siishi maisha fulani ya hivyo mimi naishi maisha ya kawaida tu.
Pamela Daffa katika pozi na Linex baada ya kipindi cha Mtu Kati.
Mwandishi: Kuna kipindi ulikuwa kama umetibuana na Mzungu, mlishamaliza tofauti zenu?
Linex: Yaa ni kweli nilikuwa na tatizo kweli na Mzungu na alivyokuja hapa tumemaliza tofauti zetu na tuko pamoja na sasa hivi yeye karudi zake Ulaya na mimi nipo Bongo maisha yanaenda.
Mwandishi: Ulimpa mimba msichana halafu ukawa hujui kama mimba ni yako, vipi mwanao sasa hivi?
Linex:  Unajua siku zote mzazi anatakiwa awe ‘proud’ na mtoto wake hata familia yake lakini kuna vitu fulani kama vinanishinda na ninajitahidi sana kutoa sapoti kwa mama yake na nilimwambia tufanye mpango kwa sababu yule mtoto mpaka leo hatumii jina langu anatumia jina la mtu mwingine na ana umri wa miaka nane mpaka sasa.
Mwandishi: Ulijuaje kama mtoto ni wako?
Linex: Unajua nimeletewa mtoto akiwa na miaka saba, nami sijakataa na wala sikutaka mambo ya DNA kwa sababu nilivyomuona niligundua ni wangu kabisa na hata mama yangu pia.
Mwandishi:  Unatoa sapoti ya kutosha kwa mwanao?
Mfanyakazi wa Global, Clarence Mulisa (kulia) akiongea jambo na Linex baada ya mahojiano.
Linex: Ninasapoti kwa kiasi kidogo kwa vitu vidogovidogo na nilimwambia mama yake kama yuko tayari tufanye mpango mtoto abadilishwe jina kwa sababu mimi ni baba yake napambana na kazi, kila siku silali muda mwingine nakesha studio narekodi kwa hiyo ninaweza kumpa maisha mazuri dogo naye asije kupita katika njia ambazo nilipita mimi.
Mwandishi: Mwanao yuko Kigoma au Dar es Salaam?
Linex:  Yupo hapahapa Dar.
Mwandishi: Ulimzingua sana mama mtoto wako mpaka akaamua kufanya hivyo nini?
Linex:  Hapana, ilivyotokea hiyo kitu tulipoteana halafu alikuwa katika mipango ya kuolewa na alivyoolewa jamaa akaja kugundua kuwa mtoto hakuwa wake wakawa wana tofauti, baadaye wakaja kuachana mtoto akiwa na miaka mitano na amekuja kunitafuta tayari mtoto akiwa na miaka nane.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top