
Miongoni
mwa matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wanaume katika suala la
kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinaonesha
kuwa, wanaume saba kati ya kumi wanakasoro hii.
Malalamiko
yanayotolewa na baadhi yao yanakariri kwamba, muda wa kumaliza tendo
huwa kati ya nusu dakika na dakika tatu kwa tendo la kwanza, huku
wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu za hamasa ya kimahaba.
Hata
hivyo kumetolewa maelezo na nafuu ya ongezeko la muda katika tendo la
pili na kuendelea, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla
ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume walio wengi.
Ndoa
na wapenzi wengi wameachana kwa kasoro hii waliyonayo wanaume. Karibu
kila kona kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na
tatizo la ufikaji kileleni mapema, ambalo limewafanya waonekane si
�keki� kwa wapenzi wao.
Ni
ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya
mwenzake humsababishia kero mwanamke anayeshiriki naye tendo, kwani
humwacha njia panda pasipokuwa na hitimisho la raha ya kujamiiana.
Hali
hii inatokana na maumbile ya mwanaume yanayomlazimisha kusinyaa uume
mara baada ya kuhitimisha mbio zake, ingawa kwa mwanamke kuwahi si
tatizo, kwani hakumfanyi ashindwe kumsindikiza mwenzake hadi kileleni.
Pengine
utofauti huu ndiyo unaowafanya wanaume wahuzunike zaidi wanapokabiliwa
na janga hilo kiasi cha kufikia hatua ya kwenda kwa waganga kutafuta
tiba ya miti shamba ili iwasaidie kuepuka balaa ya kutoka uwanjani na
aibu.
Ingawa
kumekuwa na mafanikio katika tiba asili, lakini bado wanaume
wameshindwa kupata ukombozi wa kudumu wa tatizo hili. Wengi wamejikuta
wakijiongezea mzigo wa fikra kwa kuzitumaini zaidi dawa, jambo ambalo
huwalazimisha kuzitumia kila wanapofanya tendo na ikitokea hawakuzipata,
aibu hubaki pale pale.
Kwa
kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na
madhara yachipukayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo
kwa kutumia kanuni za kisaikolojia, badala ya dawa na mafaniko yasiyo na
madhara yakapatikana.
Kimsingi
kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini.
Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa
mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mwanamke anayefaa
kimapenzi.
Inaelezwa
kuwa, akili ikishiba vigezo na kutuma taarifa zenye usahihi kwenye
mwili viungo hupokea hisia na kuanza kusumbua. Kwa msingi huo kama
tunataka kufika kileleni mapema au kuchelewa lazima tucheze zaidi na
akili kuliko mwili.
Katika
hali ya kawaida nguvu ya kupenda inayomwingia mtu huwa kubwa, lakini
suala la kupunguza ukubwa wa hisia lazima lipewe kipaumbele. Jambo kubwa
linalowasumbua wanaume wengi wenye tatizo la kufika kileleni mapema ni
kuwa na PUPA ya kufanya ngono.
Wengi
wao hupokea hisia zilizokuzwa na kwenda nazo katika ufanyaji wa tendo
la ndoa. Wataalam wa saikolojia wanasema ili mwanaume achelewe kumaliza,
lazima apunguze mhemko unaotokana na kuona, kuhisi na kupagawishwa na
staili au chombezo toka kwa mwanamke.
Anachotakiwa
kufanya ni kutumia zaidi ya dakika 20 kufanya maadalizi na mpenzi wake
kabla ya kuanza tendo. Hii itasaidia kuufanya mhemko wake ushuke na
kumuongezea muda wa kumaliza.
Aidha
mbinu ya kuidanganya akili lazima itumike ili kuzima taarifa za juu za
uzuri wa mwanamke, maumbile na raha ya starehe isipokelewe kwa nguvu
kubwa mwilini. Hii ikiwa na maana kuwa kuna kipindi inabidi fikra za
mwanume zisihamasike sana kwenye tendo badala yake iletwe mawazoni hali
ya kawaida, si ile ya kuweweseka na kuhema hema hovyo. Yafuatayo ni
maelekezo ya msingi ya kufanya, ili mtu asifike kileleni mapema:
Mume
na mke wanapoingia katika uwanja wa mapenzi wakae kwanza kwa muda, huku
wakiwa wamejiachia na mavazi mepesi. Pili wacheze michezo mingi kwa
muda mrefu bila kuanza kazi yao. Wakiwa kwenye hamasa hizo wasiwe kimya
bali wazungumze na kuulizana maswali ya kimahaba.
Baada
ya hapo mbinu nyingine ya kuzuia mbegu za kiume zisitoke ni ile ya
kujibana. Inashauriwa kuwa mwanaume akiona dalili za awali za kumaliza
bila kujali ametumia muda gani anachotakiwa kufanya ni kukaza misuli ya
miguu na kuzuia mbegu kwa mtindo atumiao kuzuia haja ndogo isitoke.
Kujibana
huko kunatakiwa kuende sambamba na kuacha kucheza �shoo�. Pacha na hilo
mwanaume anatakiwa kuidanganya akili kwa kuilazimisha iwaze jambo
jingine hasa la kuhuzunisha ili kuharibu taarifa za raha zilizotumwa
mwilini zisiendelee kufanyiwa kazi na hatimaye kumaliza tendo haraka.
Zoezi
hili linaweza kuwa gumu katika hatua za kwanza kutokana na kukosea muda
sahihi wa kujizuia, lakini mhusika akiendelea kujizoeza atajikuta
anaweza na kupata uwezo wa kufanya mapenzi hata kwa saa nzima, hivyo
kuondokana na tatizo hilo bila tiba wala madhara.