Utafiti
uliofanywa na chuo kimoja kikuu nchini Marekani, imebainisha kama
ukitaka kujua iwapo mwanamke amevutiwa na wewe, inabidi uangalie zaidi
ishara kuliko maongezi, na hii kuhitimisha wanawake huongea tofauti na
wanachomaanisha. Waulize wanaumeimekuandalia ishara kumi
zilizothibitishwa na watafiti pamoja na wanasayansi ambazo mwanamke
hufanya pindi anapovutiwa na wewe akiwa anajijua au hakiwa hajijui ili
kukuonyesha kama amevutika nawe.
Jifunze ishara hizi na maisha yako ya kimahusiano yatabadilika kwa hali ambayo hautaitarajia.
#10; Anashika au kupikicha nywele.
Kwa
zaidi ya miaka 40, watafiti wamenyumbuisha tabia wanazozifanya wanawake
kukujulisha wamevutiwa na wewe, iwapo mwanamke akizishika shika nywele
zake kwa muda mfupi inaweza kuwa ishara ya kukupa taarifa ya kuwa
anafurahia uwepo wako, ila akiendelea kuzichezea kwa muda mrefu
inawezekana akawa katika hali ya kutokujiamini au hakuamini wewe.
#9; Anauma midomo yake.
Tabia
hii mwanamke huifanya ili kuhamisha fikra zako kuelekea kwenye midomo
yake, inaweza maanisha ukienda na ukiwa mchombezaji mzuri mabusu
yanaweza kuwa ya kufikia, inabidi uwe mwangalifu sana wakati wa
kuitambua hii tabia na akiwa anauma midomo yake kwa muda inamaanisha
amevutiwa nawe ila kuuma midomo mara kwa mara inaweza onyesha ndio
mazoea yake, kwa hiyo kuwa makini kutofautisha kati ya hizo tabia mbili.
#8; Anacheka cheka, kukusumbua na kukuangalia kwa macho mazuri.
Hii
tabia zipo pande zote mbili, hata wanaume pia huifanya ila kwa wanawake
wanaweza pia kuitumia ili kukujua nia yako kwao, kwa hio usiichukulie
kwa haraka sana inawezekana anakujaribu tu.
#7; Anakukaribia sana kimwili.
Ukaribu
tunao karibia watu inategemeana na mahusiano yetu kwao, ukimkaribia mtu
sana huwa mara zote ni katika hali ya upendo,
kwahio mwanamke akikukaribia sana inawezekana akawa anafanya hivyo ili
upendezwe naye zaidi, inabidi kabla hujafanya maamuzi yeyote hakikisha
umehakikisha mkaribio wake kwako sio wa hali ya kikawaida, na unaweza
hakikisha kwa kusogea kidogo ili kumtegeshea kama atasogea tena huku
ukiwa na tabasamu usoni.
#6; Anachangia unachozungumza na kuongelea kuhusu mambo yake binafsi.
Baada
ya kufanya mazungumzo kwa muda na kunoga, jaribu kupeleka mambo mbele
kwa kuanzisha mada ambayo inahusu maisha yako binafsi ila hakikisha mada
isiwe ya ndani sana na isiwe inaelekea kana kwamba unataka kumjua kwa
undani na maelezo yake yasiwe yanamlenga, hii itamfanya ajisikie huru na
kutokuogopa, iwapo mambo yakienda vizuri na amevutika nawe utaona na
yeye anachangia kwa kutoa mada inayohusu mambo yake binafsi, watu huwa
wanaongea kuhusu mambo ya ndani kwa watu wanaowapenda na kujisikia huru
mbele yao.
Iwapo
maongezi haya mkiyafanya huku mnakula chipsi kwa pamoja itafanya mambo
yaende vizuri zaidi, kutumia vitu pamoja huongeza ukaribu na maelewano
zaidi.
#5; Anakua na urafiki wa kimaongezi wakati mnaongea.
Sahau
kuhusu mistari ya kutongozea ulioifanyia mazoezi, ikija kwenye
kuangalia hamasa ya mwanamke kwako, huangalii jinsi unavyomsifia,
unaangalia mapokeo ya maneno unayomwambia, mwanamke akikujibu hata kama
kwenye hali ya kukataa jambo, akikujibu kwa sauti ya upole na laini ujue
amependezwa nawe, kwahiyo usiwahi kuondoka kutoka katika mazingira hayo
au sehemu hio, ila akikujibu kwa sauti ya ukali, tafuta pakutokea.
Ili
kuondokana na kupoteza muda kutongoza mwanamke ambaye havutiwi na wewe,
jaribu kwa kuanza na maswali rahisi ambayo majibu yake ni rahisi, kwa
njia hii utajua kama kapendezwa na wewe au vipi, kama hajapendezwa na
wewe utaona anakuondoa kwenye maongezi ila aliyependezwa na wewe
ataendelea na maongezi.
#4; Anakua katika mkao wa mwaliko kimaongezi.
Mwanamke
akiwa amependezwa na wewe huwa anakua amekaa mkao wa mwaliko wa
kimaongezi, akikuangalia anakua na macho ya kiurafiki na si ya ukali na
hata ukiwa mbali utajua kwamba pozi na macho yake vinakuita.
#3; Anakua na ishara unazozifanya wewe.
Mwanamke
akipendezwa nawe, atakua anajibu mapokeo ya ishara zako unazotoa, kwa
mfano ukitabasamu na yeye utamuona anatabasamu vile vile, ukicheka na
yeye atakufatiliza hivyo hivyo.
#2; Anapindisha kichwa kidogo na kutabasamu.
Watafiti
wamebainisha mwanamke akipindisha kichwa kidogo na kuachia sehemu ya
shingo yake kuonekana kidogo ikifuatiwa na tabasamu mara nyingi anakua
amevutiwa na anachokiangalia.
#1; Anachezesha macho.
Kukutanisha
macho ni kitendo cha ukaribu kwa binadamu, kurudia rudia au kuendeleza
kukutanisha macho huwa kuna maana kuu mbili, kwanza kuonyesha hali
ya mguso kihisia, na pili kuonyesha hali ya jazba.
Ili
kujua kama analo hitaji la kuongea nawe, angalia jinsi anavyochezesha
na kukutanisha macho na wewe, utakuta mnakutanisha macho zaidi ya mara
kadhaa na kukiwa na tabasamu nyingi, kama ukiona mmekutanisha macho
halafu akaacha kukuangalia tena jua huyo hajavutika na wewe, na isiwe na
shaka sana maana mara nyingi kitu hichi huweza kutokea bila ya wewe
kukitambua.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Filed Under:
mapenzi
Thursday, 16 October 2014


