Mwalimu alikuwa na desturi ya kufanya mazoezi na alikuwa mtu aliyefuata masharti na ushauri aliokuwa akipewa na madaktari.
Daktari wa kwanza aliyekuwa anamhudumia Mwalimu baada ya Uhuru alikuwa ni Profesa Mhonoli. Kuanzia mwaka 1979 alihudumiwa na Profesa Makene akisaidiwa na Profesa Mtulia na Profesa Mwakyusa.
Mwalimu alipostaafu mwaka 1985 alibakia na daktari mmoja tu, Profesa Makene. Makene alistaafu mwishoni mwa mwaka 1987 na tangu wakatu huo Profesa Mwakyusa ndiye alikuwa daktari wake hadi alipoaga dunia Oktoba 14, 1999.
Profesa Mwakyusa alisema ugonjwa wa kansa ya chembe chembe nyeupe za damu, huwapata watu wenye umri mkubwa na utafiti wa kisayansi haujafanikiwa kutambua ni kitu gani hasa kinacholeta kansa hiyo. Kwa kawaida, kansa hiyo haioneshi dalili wakati inapoanza na wengi wanagundulika kuwa nayo bila kuihisi.
Alisema baada ya Mwalimu kugundulika kuwa na kansa Agosti 1998, alielezwa kuhusu ugunduzi huo na kuambiwa kuwa wakati ule ugonjwa ulikuwa haujafikia hatua ya kuhitaji matibabu. Alielezwa haja ya kwenda kupimwa mara nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa kawaida yake na kwamba hapakuwa na sababu ya kubadilisha mwenendo wa shughuli zake.
Ratiba tuliyopewa ilimfanya Mwalimu arejee London, Novemba 1998, majibu yaliyoonesha kuwa hakukuwa na sababu ya kuanza matibabu. Aidha, Januari 1999 alipimwa tena kwa mara nyingine ikaonekana hakukuwa na haja ya kuanza matibabu.
Mei 1999 alikwenda tena London akapimwa. Aliambiwa hakukuwa na sababu ya kuanza matibabu na akapewa tarehe nyingine, Agosti 1999.Safari hii hitilafu zikaonekana katika damu. Hitilafu hizo zilionesha ulazima wa matibabu ya kansa kuanzishwa.
Mwalimu alishauriwa kurudi London, Desemba 1999. Lakini hali yake ikabadilika kabla ya kurejea nyumbani hadi ikabidi alazwe katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas ambako alipoteza maisha yake Oktoba 14, mwaka 1999.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

