Habari Kali
Loading...

KAKOBE ALIVYOANZISHA KANISA NA VIJANA KUMI NA TATU -3

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


Makala: Elvan Stambuli
Naendelea kuwaletea mazungumzo kati yangu na Askofu Zakary Kakobe kuhusu alivyoanza kufanya miujiza ya uponyaji baada ya kuokoka.Mwandishi: Baada ya watu kutoamini kama ungeweza kumponya kwa maombi yule mama aliyekuwa bubu ulifanya nini?
Askofu Zakary Kakobe akihubiri.
Askofu Kakobe: Niliwaambia waende mitaani wakawaalike watu wengine ili waje waone miujiza ya Mungu kwani baada ya muda mfupi yule mama angezungumza kama kawaida na kuwika kungesimama mara moja.
Mwandishi: Je, walikubali kufanya hivyo?
Askofu Kakobe: Walikubaliana nami. Waliondoka na kwenda mitaani kuita mashuhuda na baada ya muda uwanja ulijaa mamia ya watu ambao walikuwa na shauku ya kuona muujiza ule.
Mwandishi: Je, hukutetemeka kama mwanzo na mambo yalikuwaje?
Askofu Kakobe: Sikutetemeka tena kwa sababu nilijua Yesu alikuwa pamoja nami na baada ya maombi kwa muda mfupi sana yule mama akaanza kuzungumza na kule kuwika kama jogoo kukaacha mara moja! Walingoja kwa saa nne, hakuwika na wakangoja tena kwa usiku nzima, hakuweza kuwika.
Mwandishi: Baada ya muujiza huo mambo yalikuwaje katika Kijiji cha Chalinze?
Askofu Kakobe: Siku iliyofuata wananchi wengi zaidi walifika katika mkutano wa Injili na wengi wakavutiwa na Yesu na kuamua kumfuata na iliendelea hivyo mpaka siku za kufanya mkutano pale zilipokwisha. Muujiza ule nao ulikuwa gumzo katika kijiji kile kwa miaka kadhaa baada ya mkutano ule wa Injili.
WACHUNGAJI WALIONA ANABURUDISHA
Mwandishi: Nini kilifuata baada ya mikutano yote hiyo ya Injili?
Askofu Kakobe: Baada ya mikutano kumi ya Injili sehemu mbalimbali nilimalizia mikutano hiyo Februari 1989 katika Kanisa la Kipentekoste Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo niliwasiliana na wachungaji wote wa sehemu zile kumi nilizofanya mikutano ya miujiza ili kujua kilichoendelea na kujua wale walioamua kumfuata Yesu, je walifuatilia kuona kama walimfuata kwa dhati kwa wakati wote baada ya mikutano?
Askofu Zakary Kakobe akitoa huduma ya uponyaji waumini.
Mwandishi: Jibu la swali lako kwa viongozi hao lilikuwaje?
Askofu Kakobe: Nia yangu ilikuwa kuhakikisha matunda tuliyovuna yanabaki kuwa mazuri kwani niliamini yalikuwa ni matunda ya Bwana kama ilivyoandikwa katika Yohana 15:16; 1 Wathesalonike 3: 5,8.
Nilikuja kugundua kuwa wachungaji wengi hawakuwafuatilia waumini wapya, wengi waliona kama ilikuwa ni aina fulani ya kuwaburudisha watu. Na kuthibitisha hilo ni kwamba baadhi yao waliomba likizo baada ya mikutano ile kumi.
AANZISHA KANISA LAKE NA WATU 13
Mwandishi: Ulipogundua hivyo, ulichukua hatua gani?
Askofu Kakobe: Niliamua kumtafuta tena Mungu kwa nguvu sana. Baada ya kufanya maombi kwa mwezi mmoja na nusu, Mungu alinionesha waziwazi kwamba nianzishe Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship; ambalo ataleta matunda na kuyaona yanabaki kuwa yake.
Mwandishi: Kanisa hilo ulilianzisha lini?
Askofu Kakobe: Ni kwamba Aprili 1989, nilikusanya vijana 13 nyumbani kwangu Kijitonyama, Dar es Salaam tukawa na kozi ya Biblia kwa wiki mbili. Baada ya hapo Aprili 30, 1989 nikaanzisha huduma ya kanisa katika Shule ya Msingi ya Mnazi Mmoja, jijini Dar.
Mwandishi: Baada ya hapo mambo yalikuwaje?
Askofu Kakobe: Neno la Mungu likatimia, nikawa mchungaji na baada ya siku chache nikaanza kufundisha watu Biblia.
Mwandishi: Hivi sasa kanisa lako limepanuka, je una wachungaji wangapi?
Askofu Kakobe: Nina wachungaji wengi sana zaidi ya 700 Pastors. Jumapili ya Machi 7, mwaka 1993 nilipata kundi la kwanza la wachungaji 28 na tukaweza kufungua makanisa 19 ambayo ni matawi yetu katika makao makuu ya mikoa 19 na Februari 2000 tuliweza kuanzisha makanisa zaidi ya 400 katika mikoa na wilaya zote za Tanzania Bara.
AELEZA SIRI YA MAFANIKIO
Mwandishi: Nini siri ya mafanikio hayo?
Askofu Kakobe: Siri kubwa ni moja tu, kufuata maagizo ya Mungu na kumjua kwa dhati. Mathayo 4: 18-19 anasema mshindi ni mvuvi wa watu (Mathayo 4: 18-19). Sisi ni wavuvi wa watu. Katika uvuvi, wavuvi hutumia chambo kuficha makali ya ndoano. Wavuvi kutumia uchawi wa wadudu au samaki wadogo kuficha ndoano ili kuvutia samaki.
Ishara na maajabu ya kutumia ndoano za samaki au ndoano za watu kuwavutia watu wasioamini ni kuwafanya waamini katika wokovu.
Mwandishi: Unaweza kukumbuka mikutano mingapi ya miujiza uliyowahi kuifanya?
Askofu Kakobe: Ni mingi sana na mikutano hii ilisaidia sana kupanda mbegu ya kanisa hili. Mwaka 2007 pekee nilifanya mikutano 211 ya miujiza kwenye miji na vijiji mbalimbali katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Itaendelea wiki ijayo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top