BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
"Sifa ya mkopaji ni kitu cha juu ambayo kila benki huangalia kabla ya kutoa mkopo".
Je
unahitaji mkopo?, waombaji wengi wa mikopo ya benki hukataliwa kupewa
kutokana na kutokua na uelewa wa mabenki yanaitaji nini na sifa gani!,
na hii inatokana na kutokujua mapema sifa ambazo benki huangalia kabla
ya kutoa mikopo, japo masharti hutofautiana toka benki hadi benki ila
sifa zinazoangaliwa wakati wa ukopaji zinafanana kwa benki zote.
Waulize wanaume tunaorodhesha sifa muhimu ambazo ni lazima kuwa nazo ili kupata mkopo kupitia benki yeyote ile...
Je wewe ni mteja mpya au wazamani katika benki husika?
Ili
upate mkopo, taasisi au benki itahitaji kujua kumbukumbu zako za
kibenki kutaka nyuma ulipoanza huduma ya kibenki, wataitaji kujua hili
ili kupata picha halisi ya mzunguko wa fedha kwenye akaunti yako, hii
itawapa uhakika kama wakikupatia mkopo wakupe wa shilingi ngapi na
kukupangia marejesho utakayo rejesha ya mwezi yawe ya shilingi ngapi
kutoka na uwezo wako wa mzunguko kifedha.
Je unabiashara unayoifanya?
Benki
nyingi wanapenda kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, kwa
hiyo iwapo malengo yako yalikua ya kukopa ili ujenge ni vyema kwenye
sababu ya kukopa ukatoa sababu ya kupanua mtaji wako wa biashara,
wanaangalia biashara au shughuri inayozalisha kipato zaidi ili kuwa na
uhakika wa marejesho ya mkopo iwapo wakikupatia, na kwenye biashara ni
rahisi zaidi kurudisha pesa yao maana pesa iatakua inazunguka na kutoa
faida, na lazima biashara iwe yenye mzunguko ambao unauhakika.
Je unahistoria ya ukopaji, na wapi ulitoa mtaji?
Maswali
kama haya yanaulizwa ili kujua tabia yako ya kukopa na urudishaji wa
pesa na kama ni msumbufu kwenye malipo au la, hili linawapa uhakika wa
kukujua vizuri maana wanataka kukukopa pesa yao. Na kama ni mtaji
ulianza na shilingi ngapi, hii ni ili wajue biashara yako inakuza mtaji
kiasi gani, na iwapo mtaji ulionao ni wa kukopa au kupewa.
Je ni aina gani ya biashara unayoifanya?
Ni
lazima watake kujua ni aina gani ya biashara unayoifanya, na lazima
waje waitembelee na kuiona. Na watataka kujua mzunguko wake wa hio
biashara ulionayo na inatengeneza faida kiasi gani, na kama utakua
unaifanyia hesabu kila siku hii itakuweka kwenye manufaa zaidi ya kupewa
mkopo, yote haya yanafanyika ili benki ijue unafaa kupewa mkopo wa
kiasi gani!.
Je biashara yako inamtaji kiasi gani?
Benki
lazima ijue mtaji wako ulionao na mara nyingi hawawezi kukupa pesa
iliyo zaidi ya mtaji wa biashara ulionao, na hata kama wakikupatia
lazima waone kwanza hesabu ya biashara yako ili kujua mzunguko ulionao
kama unaweza kutosha kulipa marejesho yanayoendana na kiasi cha mkopo
ulioomba, hivyo ufanya hesabu kwenye biashara unakuweka katika hali
nzuri ya kupewa mkopo.
Dhamana
Benki
lazima iangalie dhamana ulionayo, na sio mpaka iwe nyumba mabenki
mengine wanahitaji dhamana ya vitu ulivyonavyo, hata kama ukiwa umepanga
unaweza kupewa mkopo, ila kwa mfano wa vitu vya ndani wakija
kuthaminisha, kama TV umeinunua kwa shilingi laki moja, kwao itakua na
thamani ya elfu hamsini!, kwa hio kila kitu kitakua nusu ya thamani ulio
nunulia.
Mdhamini
Mara
nyingi hii inafanya kazi iwapo utakua hauna nyumba na umepanga, hivyo
itakubidi umatafute mdhamini ili akudhamini na sharti atakalopewa
mdhamini lazima akubali kulipa marejesho yako ya kila mwezi ya mkopo
iwapo tu kama wewe yatakua yamekushinda kulipia, na ukiwa na nyumba,
nyumba yako ndo itakua mdhamini wako.
Mkataba wa pango la biashara
Iwapo
hapo unapofanyia biashara ni pango ambalo umepangishwa, itabidi upeleke
benki kopi ya mkataba wa hio sehemu husika na hutumika kupigia hesabu
za faida yako ya mwezi ukiwa imeshatoa na kodi yako ya pango.
TIN number yako
Utahitaji uwe na tin namba yako ya kukutambulisha kama mfanyabiashara uliosajiliwa na serikali.
Mkataba wa pango la kuishi
Iwapo umepanga, utahitajika kupeleka na mkataba wa sehemu unayoishi.
Kitambulisho cha mpiga kura
Benki
itahitaji kitambulisho chako na cha mkeo/mumeo kama umeoa/olewa ili
kudhibitisha utambulisho wako na wa mwenza wako ambae atakua kama
mdhamini wako.
Barua ya mwenyekiti
Benki itahitaji barua toka kwa mwenyekiti ili kuhakiki makazi unayoishi na kama hujafungu akaunti itatumika kufungulia akaunti.
Hayo ndo masharti ambayo Zee La Udaku tumekuandalia na sifa mabenki yanazoitaji, zingatia na hutokosa mkopo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Matukio
Wednesday, 15 October 2014