Vielelezo zaidi ya vitatu vinaonesha kuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu alidanganya umri wake wa kuzaliwa.
Vielelezo
hivyo vinaonesha kuwa mrembo huyo ana umri wa miaka 25, na sio 23 kama
cheti chake ambacho kinaaminika kughushiwa kisemavyo. Passport yake,
leseni ya udereva na taarifa za website rasmi ya ‘Idara ya Usalama wa ndani ya Marekani (Department of Homeland Security), pamoja na profile yake kwenye mtandao wa exproletalent.com vinaonesha kuwa alizaliwa May 31, 1989 na sio May 31 1991.
Passport ya Sitti Mtemvu
Sitti
alilazimika kupunguza miaka yake ili kwendana na sharti la mashindano
ya Miss Tanzania yanayotaka mshiriki awe na miaka kuanzia 18 hadi 24.
Hivyo kutokana na vielelezo hivyo, Sitti Mtemvu ana asilimia 100 za
kuvuliwa taji na kupewa mshindi wa pili.
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu
Kama
uamuzi ambao kwa sasa upo mikononi mwa Baraza la Sanaa la Taifa, BASASA
na wizara husika utakuwa vingine, huo utakuwa mwanzo wa kushuka kwa
uhalali wa mashindano hayo pamoja na sifa za mamlaka hizo. Dalili za
kuwepo udanganyifu huo, zilizoongezeka zaidi pale Mtemvu alipokutana na
waandishi wa habari ambapo pamoja na kuwashutumu kwa kuandika habari za
uongo, maelezo yake yalikuwa na walakini.
Maelezo
ya I-94 hupatikana kwa mtu yeyote kupitia website ya Department of
Homeland Security. Kama unahitaji kupata taarifa ya safari za mtu nchini
Marekani, andika majina yake, tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, nchi
alipopata passport yake na namba yake ya passport, utapewa taarifa hiyo
“Ukweli
ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka
mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti.
Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea akidai kuwa
ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara
“Kwahiyo
ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea.
“Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,”
alijibu mrembo huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti
yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo.
Taarifa za Sitti Mtemvu kwenye exproletalent.com zinaonesha kuwa ana umri wa miaka 25
Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.
Sitti
alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto,
na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa
mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.
Akijibu
swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka
1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31,
1991, Sitti alisema:
Sitogusia
hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’
niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life,
kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu,
ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni
kitu ambacho mngependelea.”
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim
Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri na
maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi.
“Tukishapata
proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi
hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema
Lundenga.
BASATA
imepewa siku saba kufuatilia ukweli juu ya umri wa Sitti Mtemvu, na kwa
vielelezo hivyo visivyojificha, hakuna shaka litakuja na uamuzi sahihi,
kumvua taji hilo.