BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
1.
Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni
kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana
sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama
akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine
kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli,
utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio
yaote ganzi.
2.
Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa
na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni
kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda
atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka
nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.
3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo,
hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati
mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani
amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea
kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.
4.
Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na
wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo
mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi
kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka
kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna
lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika
tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye
kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo
mnalojadili kwa wakati huo tu.
5
Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo
umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona
nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya
hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya
hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,'
kabla ya visasi hivyo.
6 Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya
kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama
hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya
kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya
kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako
mabaya dhidi yake.
7 Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna
jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo
fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa
moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe,
anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.
8 Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo
fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akikuambia, 'asante
sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na
bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida.
Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza
kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi
kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi
usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Thursday, 16 October 2014