Watu
wengi wamekuwa wepesi kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa
mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi waliyonayo. Imani iliyojengeka kwa
watu wengi katika jamii yetu ni kuwa, ushauri ni kitu muhimu sana kwa
kila hatua.
Kwa
mtazamo wa haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na
kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi.
Unapokerwa na mpenzi wako unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata
unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
Je,
umeshawahi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki
yako? Hebu soma hapo chini ujue baadhi ya hasara za kusikiliza ushauri
wa kimapenzi kutoka kwa rafiki yako......
1.UTAKUPOTOSHA
Ni
wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi
mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza
kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea
suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.
Uchunguzi
unaonesha kuwa, wapenzi wengi hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na
uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vyema
kuwa makini unaposhauriwa na rafiki yako.
2.UTARAHISISHA MAMBO Mara
nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi
kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi.Anaweza
akasema maneno kama haya hapa chini......
“Vipi kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.
“Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa
mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye
utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu
ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge
mwenye kuumia utakuwa ni wewe.
3.UTAKUGEUZA Ulimwenguni
kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa
staili yake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya
mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo.
Uzoefu unaonesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini
je, ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?
Jibu
ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya
mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze, aamue na apende kama staili
yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke
ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu
lakini upime kama unalingana na matakwa yako.
4.UTAKUONDOLEA UJASIRI
“Kwa
maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha,
ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
Huu
ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na
tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake
mbaya.
Ushauri
huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri
atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi.
Ikumbukwe kuwa, anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama
mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka
jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi
alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.
5.UTAKUNYIMA FURSA
Kwenye
mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa
mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa
usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.
N.B:
Siyo kwamba ushauri kutoka kwa rafiki yako ni mbaya,, hapana..!!! bali
unatakiwa kuangalia huo ushauri na matakwa yako mwenyewe...
Credit: habarizetuleo.blogspot.com