BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Hospitali kongwe ya Wilaya ya Kisarawe
mkoani Pwani, inakabiliwa na upungufu wa wodi za kulaza wagonjwa na
kulazimika kuwachanganya wagonjwa wenye matatizo ya akili na wale wenye
maradhi mengine.
Muuguzi wa hospitali hiyo, Bahati
Kuguru, alisema hospitali hiyo ni miongoni mwa zile zinazofanya kazi
katika mazingira magumu hasa ya kutokuwa na wodi maalum za kulaza
wagonjwa hali inayohatarisha usalama wa wagonjwa na wauguzi.
“Serikali iangalie namna ya kunusuru
hali hii haraka iwezekanavyo kwa sababu wagonjwa wenye matatizo ya akili
kitabibu wanahitaji kulazwa wodi maalum peke yao, vinginevyo wanaweza
kuleta madhara kwa wagonjwa wengine na wauguzi pia,” alisema Kuguru.
Pia alisema chumba cha kuhifadhia
wagonjwa cha hospitali hiyo ni kidogo na hakina majokofu jambo
linalosababisha ndugu kulazimishwa kuchukua miili ya ndugu zao muda
mfupi baada ya kufariki dunia.
Aliongeza kuwa ingawa serikali
inazitambua changamoto zilizoko, bado haijashirikiana na hospitali hiyo
katika kuboresha mazingira halisi badala yake miundombinu yake inazidi
kuchakaa.
“Tunaomba serikali ichukue maamuzi
magumu katika kutatua suala hili, kwanza itupatie gari ya usafiri
itakayotumika kutoa huduma ndani na nje ya hospitali pale inapobidi
pamoja na kujenga majengo yatakayojitegemea kutokana na tatizo la
wagonjwa,” alisema Kaguru.
Mgonjwa wa matatizo ya akili aliyelazwa
katika wodi ya wananwake katika hospitali hiyo, Roida Mwangaya, alisema
serikali iboreshe hospitali hiyo kwa sababu ni kitovu cha wakazi wa
ndani na nje ya eneo hilo.
“Ipatikane wodi maalumu za kulaza
wanawake, watoto, wanaume pamoja na kitengo maalum cha kuwalaza na
kuwalea wagonjwa wa matatizo ya akili,” alisema Mwangaya.
CHANZO: NIPASHE
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Kitaifa
Thursday, 16 October 2014