Habari Kali
Loading...

FLORA MVUNGI AKIRI KUUZA NYAGO BILA MALIPO

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

BAADA ya kumaliza kusoma Exclusive Interview ya msanii mkongwe wa filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ leo katika safu hii tunamleta kwenu msanii wa filamu na muziki, Flora Festo Mvungi.

HISTORIA KWA UFUPI
Staa huyu amezaliwa mwaka 1988 katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya wanne waliozaliwa katika familia yao.Amesoma Shule ya Msingi Mpakani iliyopo Mabibo baada ya kuhitimu alijiunga na kidato cha kwanza hadi cha nne Makongo Sekondari.
Baada ya kuhitimu kidato cha nne alijiunga na kidato cha tano na sita katika shule ya Tegeta High School. Hapa chini anafunguka maswali aliyoulizwa na mwandishi wetu.
Mwandishi: Baada ya kuhitimu kidato cha sita, ulienda wapi au ulijishughulisha na nini?
Flora: Baada ya hapo nilijiunga na Chuo cha Uandishi wa habari, Royal na kuchukua diploma ya uandishi na utangazaji.
Mwandishi: Baada ya kumaliza chuo ulifanya kazi ya uandishi kwa muda gani na wapi?
Flora: Nilienda kufanya field Mwananchi nikashindwa kwa miezi miwili tu.
Mwandishi: Uliingiaje katika masuala ya ulimbwende?
Flora: Nilipohitimu kidato cha nne nilishiriki kwenye mashindano mbalimbali ya u-miss ambapo nilianza na Miss Bagamoyo na kufanikiwa kutwaa taji hilo, nikashiriki Miss Pwani nikatwaa taji, nikashiriki Miss Kanda ya Mashariki nikapata taji, Miss Dar Talent, mwisho nilishiriki Miss Tanzania lakini sikutwaa taji na haya yote ilikuwa ni mwaka 2008.
SANAA
Mwandishi: Kwenye sanaa ya filamu uliingiaje?
Flora: Tangu nikiwa mtoto nilikuwa napenda sana filamu hivyo baada ya kumaliza kwenye mambo ya umiss nilikutana na Kulwa Kikumba ‘Dude’ maeneo ya Magomeni, Lango la Jiji ambako wasanii wa vikundi mbalimbali walikuwa wakikutana kwa ajili ya mazoezi.
Baada ya kukutana naye ndipo nikamweleza kwamba ninapenda kuingia kwenye sanaa akaniambia niende siku inayofuata kwenye kikundi chake kilichokuwa kinajulikana kwa jina la Splended Ilala.
ACHUKUA FOMU
Mwandishi: Nini kilichoendelea baada ya hapo?
Flora: Kesho yake nilienda nikapewa fomu nikajaza na kuanza mazoezi rasmi.
KUNDI LASAMBARATIKA
Mwandishi: Ulikaa kwenye kikundi hicho kwa muda gani?
Flora: Nilikaa kwa miezi miwili kundi likasambaratika ndiyo baada ya hapo Dude akakutana na Mrisho Mpoto ambapo walitengeneza wazo la kuanzisha Kundi la Bongo Dar es Salaam.
Baada ya kuanzisha Kundi la Bongo Dar es Salaam niliendelea kuigiza na Dude japokuwa mwanzoni ilinipa shida sana.
KUIGIZA UTAPELI
Mwandishi: Kuigiza utapeli kwenye Bongo Dar es Salaam haikuwa ngumu kwako?
Flora: Yaani kuigiza utapeli ilikuwa ngumu sana mwanzoni lakini Dude ndiye alikuwa akinifundisha hasa zile alama za utapeli kwa kutumia macho pia jinsi ya kutembea.
Kutokana na kuigiza utapeli hapo ndipo umaarufu wangu ulipoanzia ambapo Bongo Dar es Salaam ilikaa kama miaka mitatu tu ikapotea.
MALIPO
Mwandishi: Je ulikuwa ukilipwa shilingi ngapi?
Flora: Kwa kipindi hicho kwa sababu nilikuwa nataka nijulikane nilikuwa silipwi chochote nilikuwa nauza jina na sura tu wala sikuwa naona shida yoyote.
KUONEKANA RUNINGANI
Mwandishi: Siku ya kwanza kuonekana kwenye TV ulijisikiaje?
Flora: Ukweli nilikuwa na raha sana kila mtu mtaani kwetu na ndugu zangu walijua kwani niliwapa taarifa kwamba waangalie TV.
AKUTANA NA MWAKALEBELA
Mwandishi: Baada ya Bongo Dar es Salaam ulifanya kitu gani?
Flora: Nilikuwa napenda sana mpira wa miguu sasa siku moja nikiwa Uwanja wa Taifa nikiangalia mechi, mdau wa soka, Frederick Mwakalebela akaniambia anataka kuanzisha kampuni ya filamu lakini hajui aanzie wapi ndipo nikamuunganisha na Dude.
Baada ya kumuunganisha ndipo tukacheza filamu ya Septemba Eleven ambayo ndiyo filamu ya kwanza kucheza chini ya kampuni hiyo nikiwa muhusika mkuu.

AKUTANA NA LAMATA
Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Flora: Kutokana na kucheza filamu hiyo nilijuana na mastaa wengi ambapo Wolper aliniunganisha na Lamata (Leah Richard) ambaye alikuwa akifanya kazi na Kampuni ya Daniel Basila (aliyekuwa mume wa Bahati Bukuku) nikacheza filamu iliyojulikana kwa jina la Passion.
Itaendelea wiki ijayo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top