Uchunguzi
unaonesha kuwa, wanawake/wanaume wengi husumbuka sana kutafuta njia za
kukatisha uhusiano wao wa kimapenzi na wapenzi wao baada ya kugundua
kuwa hawako kwenye chaguo sahihi kwa sababu moja au nyingine....
Wengi
wao hujikuta wanashindwa kufikia lengo hilo kwa sababu ya kutoeleweka
na wapenzi wao. Dondoo za mahojiano zilizofanyika kwa baadhi ya
wanawake zinaonesha kuwa, asilimia 48 kati yao wanaishi kwenye mapenzi
ya lazima au yaliyowachosha.
Utakuta wanawake wengi wanasema maneno kama haya hapa chini.....
“Sina
la kufanya, nimemwambia mara nyingi tuachane lakini hasikii, ananitisha
kuwa nikimwacha atanikomesha. Anachofikiri nimepata mwanaume mwingine
lakini ukweli tabia zake zimenichosha,”
Kisaikolojia
mapenzi ya kulazimisha nafsi yamekuwa na madhara makubwa kiafya na
kiufahamu. Wengi kati ya watu waliotokea kuua, kujiua au kujeruhi
wanatoka katika kundi la maisha ya mapenzi ya lazima.
Chukua hatua zifuatazo kama umeamua kuachana na mpenzi wako uliyemchoka.
1. KUWA MKWELI
Wanawake/wanaume
wengi wamekuwa wakificha sababu za kutaka kuachana na wapenzi wao
wakihofia kuwaumiza au kujiumbua. Ukweli unamtaka mwanamke amwambie wazi
mwanaume kwa nini anataka kukatisha uhusiano. Mweleze ajue kasoro zake
na uweke wazi hali ya kuchoka kumvumilia kuwa nae.
2. MUDA SAHIHI
Usikurupuke
kuachana na mpenzi wako. Lazima uhakikishe kuwa uko kwenye wakati
sahihi ambao hautakufanya ujutie uamuzi wako. Ikiwa unajua kuna gari
umemuazima, pesa, mali na vitu vingine vya thamani tafuta njia za kuzuia
visipotee. Ushauri wa kitaalamu kuhusu mali ni muhimu ukauzingatia
kabla ya kuamua.
3. SHIRIKISHA WATU
Ukiwa
umehakiki mawazo yako usimwambie mhusika mkiwa chumbani. Weka wazi
azimio lako mbele ya rafiki na ndugu. Faida za kufanya hivi ni kuweka
ushahidi na wakati huo huo kumharibu kisaikolojia asiweze kurudi kwako
kwani wanaume wanatajwa kuwa na aibu ya kuonekana wanang’ang’aniza
penzi.
4. FANYA MWENYEWE
Suala
la kuachana ni binafsi, hivyo unapofikia hatua hiyo lazima uwe ni wewe
uliyeamua kufanya hivyo na isiwe shinikizo kutoka kwa watu wengine kwa
masilahi yao. Kama "ulivyopenda" ndivyo "uache".
5. UMAANISHE
Kuna
wanawake/wanaume ambao hutangaza kuwaacha wapenzi wao, lakini
hawamaanishi sawa na uamuzi wao. Utakuta pamoja na hatua hiyo huendelea
kuwatumia meseji za mapenzi, kujichekesha chekesha, kujipitisha pitisha
na wakati mwingine hata kujipeleka nyumbani. Kufanya hivyo hakuwezi
kuleta matokeo sahihi.
6. USIRUDI NYUMA
Uamuzi
wa kuachana lazima uwe umeshiba sababu ili isijitokeze hali ya kurudi
nyuma na kujuta. Mwanaume ukishamtangazia kumwacha, halafu akaona
unajirudisha mwenyewe utamfanya aamini kuwa huna pa kwenda na hivyo kama
alikuwa anakutesa na kukudharau ataongeza zaidi. Utakuwa uni kama
unasukuma ukuta wakati upo ndani ya nyumba.
Hizi
ni baadhi ya kanuni kati ya nyingi ambazo unaweza kuzichukua ili
kuachana vizuri na mpenzi wako ambaye unahisi umemchoka kwa sababu moja
au nyingine......