Habari Kali
Loading...

BEBI KUNA MJINGA KANIGONGA!

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Timbwili lililotokea juzi, ndiyo lile hasa linaloitwa nguo kuchanika. Maana zilianza ngumi za pande tatu. Ikawa hata haieleweki nani anamtandika nani, kutokana na mkasa mzima, sisi wananchi wema ililazimika tukae pembeni tumekodoa macho, tukiwa hatuelewi tufanye nini.
Sababu ya timbwili hili mimi kama raia mwema nasema lilianzishwa na ubovu wa barabara, najua wengine mtakuja kusema barabara haihusiki lakini ki-ukweli barabara ingekuwa nzuri kusingekuwa na tatizo lililotokea.  Katika kukwepa mashimo makubwa kadhaa yaliyokuwa barabarani ghafla gari mbili zenye vioo vyeusi tii wala humuoni mtu ndani zikajikuta zimegongana katikati ya barabara.
Magari husika yalikuwa ki-Vitz kidogodogo kilichokuwa kimeanza kuchoka  na Land-cruiser moja mpya ya bei mbaya. Madereva wa gari zote wakafungua milango na kutoka kumbe wote wanawake. Huyu mama dereva wa Ki-vitz  alionekana kuwa na umri mkubwa kuliko mwenzie na hata nguo zake zilikuwa za staha, alionekana kama vile ni mama mwenye hadhi kidogo anayejiheshimu ambaye ana familia na mambo yake si mabaya.
Huyu mwingine mwenye Landcruiser kubwa kama la waziri, alitoka kwenye gari na kikaptura kidogo ambacho hata mtoto mdogo kingembana, na ndiye aliyeanza kelele akionekana kuwa ni wazi atamlamba makofi Mama Ki-vitz wakati wowote.
Ubishi wa kosa la nani ulipamba moto, japokuwa wote tulijua kosa ni la Kikaptura, ila yeye ndiye aliyekuwa mkali na kudai kagongwa.Mama Ki-vitz akanyanyua simu na kumpigia mumewe, “Baba John nina tatizo nimegongwa hapa Sinza naomba uje tafadhali’.
Baba John alijibu mkato, “Jamani niko bizi hebu kaeni kikao ulisovu mwenyewe”.
Wakati huohuo Binti  Kikaptura naye si akapiga simu, “Bebi kuna mjinga  mmoja kanigonga hapa Sinza, come please”
Haikuchukua muda Bebi akafika pale, hapo ndipo picha likaanza, kumbe Bebi ndiye Baba John mume halali wa  Mama Ki-vitz!!!!
Kimsingi mwisho wa picha, Baba John akamnyang’anya kikaptura funguo za gari na kumkabidhi mkewe mbele yetu jasho jingi likiwa linamtoka.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top