MY God! Katika
hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda,
Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa
sebule yao.
Marehemu Focus Saimoni (9) enzi za uhai wake.
Baba mzazi wa marehemu Focus Saimon (9).
Focus
aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu,
amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la
mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati
wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa
nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa
siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo
wake, Irene Steve (5).
Mama mzazi wa Focus Saimoni (kushoto) akihuzunika kumpoteza mwanaye.
“Alipofika
alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia ndani, akanywa
chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na kumkuta tayari
ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
Mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria (kushoto) akiwa na mama mzazi wa Focus Saimoni.
“Nilimwambia
Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi, nilipomwangalia vizuri
ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa mama mdogo anayeishi
jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza
na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye
hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni
nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila mimi
naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema
wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya
komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.
Mdogo wa marehemu Focus Saimoni, Irene.
Akizidi
kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa
wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili umeshushwa
chini.
“Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya
mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili
umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna
aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa
nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Marehemu Focus Saimoni (9) enzi za uhai wake.
’’Tukio
hili lina shaka ndani yake, mtoto wa miaka 9 anawezaje kujinyonga, kwa
stress zipi? Kwa kweli inasikitisha sana, jeshi la polisi lina wajibu wa
kuchunguza ukweli wa kifo cha mtoto huyo,” alisema mama huyo.Baadhi ya
wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio
hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.