Ni
tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya
kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye
mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya
kukujuza.
Mastaa
watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.
KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru
za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya
kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte
alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses
Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka
maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye
Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto
mmoja.
Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.
AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah!
Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi
ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni
mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa
sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa
Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana
uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na
yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.
Alisema
kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu
waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na
alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini
nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale
anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja
kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?”
alihoji Said.
‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.
WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi
ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim
‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa
ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika
pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’
ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa
wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo
mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau
mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi
karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti
wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa
mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika
maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve
alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima
uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua
wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti
na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani
wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve
akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.
'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.
NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea
kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt
kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa
Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye
(Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua
hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao wa
Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama
unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze
Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe
anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.
AUNT AWA MBOGO
Baada
ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia
Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme
nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi
wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond
unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt
akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.
KUTOKA IJUMAA
Ni
kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’
kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe
ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.