BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Mtandao wa Instagram unaohusisha uwekaji picha umeendelea
kupata mashabiki wengi nchini Tanzania lakini wengi kati ya watumiaji
hao wameisababisha kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya
mtandao huo duniani kote.
Ripoti hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasialiano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy katika mahojiano maalum
aliyofanya na Ibrahim Issa wa 100.5 Times Fm.
“Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeongoza kwa watu kulalamika
kwamba matumizi yetu hayaendani na makusudio. Na hii inatokana na pale
watu ambao wanawafuata watu wa` Tanzania kuona vitu wanavyoweka vitu
wanavyoweka, ugomvi, matusi, picha za ajabu…za ngono na nini. Sasa watu
huwa wanalalamika.” Amesema Innocent Mungy.
“Wanapolalamika, ule mtandao huwa unaweka record kwamba watu wengi
waliolalamika kwenye mtandao huu kuhusu picha za watumiaji ambao wako
Tanzania labda ni 20 wakilinganisha na sehemu nyingine ambazo idadi
inakuwa ndogo zaidi.” Ameongeza.
Amefafanua kuwa kwenye mitandao yote ya kijamii, wakati wa kujiunga
mtumiaji hupewa maelezo ya kurasa kadhaa kuhusu namna ya kutumia mtandao
huo ikiwa ni pamoja na makatazo lakini watumiaji wengi wa Tanzania huwa
hawayafuatilii/huyapuuza.
Mwisho, Mungy ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini kuitumia mitandao hiyo kwa maendeleo na sio vinginevyo.
“Mitandao hii ya kijamii kama mawasiliano ni maendeleo. Matumizi ya
mitandao sio mabaya ila watumiaji ndio wanafanya vitu vibaya.
Ningewataka watanzania ambao wanatumia mawasiliano haya vibaya waache.
Tuitumie vizuri.
"Na wale watu ambao unawaona wewe hawaendani na matumizi
ambayo yanapendeza, wafute kwenye mtandao wako. Wa-Unlike, wa-Unfriend
au wa-delete kabisa ili usione hayo mambo yao ya kipuuzi wanayofanya.”
Credit: Ibrahim Issa (Times Fm)
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
Matukio
Wednesday, 10 September 2014