MTANGAZAJI wa
Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini
Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia
uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho, Loveness Malinzi ‘Diva’ akipozi.
Katika
mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema
anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo vya Global Publishers)
kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati
kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
MSIKIE DIVA
“Ninyi
mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi
nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini
kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa
kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: “Sasa
ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja
kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha
kirahisirahisi tu.”
KIPINDI CHAZUA BALAA
Diva
alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni
kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East
African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.
Mh. Zitto Kabwe akiwa kazini.
HASIRA ZA DIVA
Ilidaiwa
kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva
hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail
aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka
wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.
E-MAIL ILIVYOSOMEKA:
“Unanikosea
sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa
kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.
“Ungekuwa
unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa.
Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
SWALI LA MWANDISHI
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
SIKU ZA KARIBUNI
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.
KUHUSU DIVA
Kufuatia
Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa
Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake,
baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na
mtangazaji huyo.
Wengi
walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi
kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.“Sasa Diva
anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?”
Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
Naye
Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo
vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson
Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah
Monroe.“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si
msafi kivile,” alisema Ismail.
ZITTO ASAKWA
Kufuatia
madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa
njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa
alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.
Ilibidi Amani limtumie
e-mail na kumuuliza anachosema kuhusu madai ya Diva lakini kwa zaidi ya
siku kumi sasa hajajibu chochote licha ya kumfikia.E-mail iliyotumwa
kwa Zitto, Septemba 2, mwaka huu ilikuwa na kichwa cha utambulisho
kisemacho; Mambo ya Diva.
E-mail yenyewe iliandikwa hivi: A. Alaykum,
issues
za Diva zimekuwepo muda mrefu sasa. Mitandaoni hali inazidi kuwa mbaya.
Nimeshasimamisha stori isiandikwe ili useme mpaka naonekana adui wa
habari.Naomba uzungumze kitu tuone inakuwaje hii kitu kusafisha
atmosphere (upepo). Kukaa kimya si suluhu.