KAMA ndivyo, huenda Bunge Maalumu la Katiba, linalotarajiwa kuanza awamu ya pili ya vikao vyake keshokutwa mjini Dodoma, litafanyika bila ya kuwa na wajumbe kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Hali
hiyo inatokana na kauli ya Ukawa, inayoundwa na viongozi wa vyama vya
siasa vya upinzani na wafuasi wao, kwamba hawatashiriki katika Bunge
hilo na kwenda mbali zaidi, wakidai hawana mpango wa kuwa na vikao vya
maridhiano dhidi ya wenzao wa chama tawala, CCM baada ya kikao kingine
cha juzi, kilichokuwa cha nne, kukwama.
Kauli
ya Ukawa ilitolewa jana, mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa
vyama vya siasa vinavyounda umoja huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Kwa
pamoja, walisema wameridhia kujiweka kando katika Bunge na vikao vya
maridhiano. Chama cha NLD kinachoongozwa na Dk Emmanuel Makaidi, nacho
kimejiweka kando.
Mbowe
alifafanua kuwa baada ya kikao cha nne cha maridhiano kati ya umoja huo
na CCM, kilichofanyika juzi chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi kuvunjika, wametafakari kwa kina na kubaini kurejea
bungeni kuendeleza mivutano, hakutakuwa na tija kwa Taifa.
“Hivyo
tumeazimia kutorejea tena katika Bunge la Katiba wala kushiriki
mazungumzo yoyote kuhusu suala hilo, kutokana na ukweli kuwa mazungumzo
haya yaliyovunjika, yalikuwa ya kuwezesha kupata Katiba bora, lakini CCM
waliyafanya kuwa yenye maslahi ya chama chao, siyo Taifa.
”Na
baada ya awamu nne za vikao vya mazungumzo kati yetu na CCM, Ukawa
tunatangaza kwamba hatuko tayari kuendelea na mazungumzo na CCM wala
kurudi katika mkutano wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa kuwa kufanya hivyo
ni kusaliti maoni ya wananchi na kutumia vibaya fedha za umma,” alisema Mbowe.
Kauli
ya CCM Hata hivyo, kwa mara nyingine jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema chama chake
hakijashangazwa na uamuzi huo, kwa kuwa walifahamu Ukawa hawana hoja za
msingi, hivyo wamekimbia aibu.
“Hata
kwenye vikao, hawakuwa na kitu kipya, ni malalamiko tu huku wakishindwa
kujenga hoja, kwa hiyo tulijua hawa wenzetu lazima mwisho wa siku
wakimbie aibu yao…ni aibu tu imewashika, ndiyo maana wamepatafuta pa
kutokea,” alisema Nnauye.
TUCTA
na Katiba mpya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA),
Nicholaus Mgaya amezungumzia Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma
wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanawake wa shirikisho hilo.
Mgaya alisema anasikitishwa na mwenendo wa Bunge hilo, ikiwemo kwa wajumbe wake kushindwa kufikia muafaka.
“Sisi
tuna wawakilishi wetu 19 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ila
tunasikitika baadhi ya wajumbe wameacha kujadili mambo tuliyowatuma,
tungependa wajumbe wa Bunge hilo wajikite kwenye kujadili rasimu
iliyopo, waachane na matusi na kejeli,” alisema.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >


