Habari Kali
Loading...

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LEO NDIYO LEO TAIFA

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa, hatimaye imewadia ambapo leo (Agosti 8, 2014) tamasha kubwa la Usiku wa Matumaini litatingisha kinomanoma ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, burudani ya nguvu ikitarajiwa kuongozwa na mkali wa songi la Johnny, Yemi Alade kutoka nchini Nigeria.
Ali Kiba.
ALLY KIBA
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni  Mwana na Kimasomaso.”
R.O.M.A Mkatoliki,
BONGO FLEVA
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto, wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya Bongo watakinukisha wakiwemo Ali Kiba, Navy Kenzo (Nahreel na Aika), Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Madee, R.O.M.A Mkatoliki, Meninah, Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, mshindi wa Shindano la Amani Talent Search, Paschal Dominick ‘P-Plan’ na Scorpion Girls (Jini Kabula na Isabela).
SOKA
“Kutakuwa na mechi kali za mpira wa miguu kati ya Timu ya Azam FC dhidi ya wakata miwa wa Turiani, Morogoro, Mtibwa Sugar kuwania Ngao ya Matumaini, pia wabunge mashabiki wa Yanga watakipiga dhidi ya wenzao wa Simba huku timu ya Bongo Movie itapepetana na Bongo Fleva,” alisema Maloto.
NDONDI
Kwa upande wa ndondi, Maloto alisema kuwa Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba atazichapa na Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala,  mwanamuziki Khalid Chokoraa atazichapa ulingoni na Said Memba huku Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Thomas Mashali akizitwanga na ‘mbunge mtarajiwa’, Mada Maugo.
Meninah
MENINAH
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”
R.O.M.A
“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao, ukikosa utajilaumu.”
WOLPER
“Nimefanya mazoezi ya kutisha, kwa kifupi nimejiandaa kumkalisha mtu chini. Njooni muone ngumi za Kitom Boy.”
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu ambayo sijawahi kuifanya popote, si mnajua zangu ninapokuwa jukwaani, yani leo ndiyo leo.”
MADEE
“Pale taifa leo nitadhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, mbona itakuwa balaa!”

Navy Kenzo.
NAVY KENZO
“ni siku ya burudani mwanzo mwisho, tutafanya makamuzi ya kufa mtu, kikubwa ni kila mtu kufika maana haitanoga kama utasubiri kusimuliwa.”
JUMA NATURE
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay dee, Kama Jana.”
BONGOMUVI
“TutawapIgIsha kwata Bongo Fleva, huwa sisi haturembi na soka letu linajulikana kwa hiyo wajiandae kupokea magoli yakutosha. Hapa JB, pale Steve Nyerere bila kuwasahau Cloud, Dokta Cheni na wengine kibao, watu waje kuona soka la Kijerumani.”-Ray
BONGOFLEVA
“Tutacheza soka la kimataifa. Niwahakikishie tu kwamba, leo Bongo Muvi watatoka uwanjani wakiwa wameloa mvua ya magoli. Hebu fikiria wachezaji kama vile KR Mulla, Tunda Man, Kalapina na mastaa kibao, hebu vuta picha!”-H.Baba
Kikosi cha Wabunge wa Yanga.
WABUNGE
simba“TUnataka kurejesha heshima, mwaka jana wale wa Yanga walishinda ushindi mwembamba sana ila safari hii tumefanya mazoezi makali na niwahakikishie tu kwamba, Yanga safari hii watalia uwanjani.”-Idd Azzan
WABUNGE
yanga
“tumejipanga wachezaji wote wako vizuri. Sisi huwa hatuna maneno mengi, sisi ni soka tu na usajili wa mwaka huu ni balaa kwa hiyo ushindi ni lazima, watu waje waone soka lililokweda shule.”-Mwigulu Nchemba.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top