Wakati
baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kupigana
vikumbo kuwania urais wa 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba,
amesema ameombwa na watu mbalimbali wakiwamo wazee na wasomi kuwania
nafasi hiyo.
Hata hivyo, Nchemba amesema kwa sasa hafikirii suala hilo kwani amebanwa na utekelezaji wa jukumu alilokabidhiwa na Rais.
Nchemba,
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, aliyasema hayo
jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini.
Alisema
amekuwa akipokea ujumbe mwingi kutoka kwa wazee wa kijiji cha Butiama,
mkoani Mara na kutoka kwa vijana wa vyuo vikuu wakimuomba awanie urais
mwaka 2015, lakini suala hilo haliwekei umuhimu.
Badala yake, alisema anatekeleza jukumu kubwa alilopewa na Rais la Naibu Waziri wa Fedha.
Wakati
Nchemba akitoa kauli hiyo, zipo taarifa kuwa aliwaalika makatibu wa CCM
wa wilaya kutoka mikoa 11 kuhudhuria mkutano aliokuwa ameundaa jijini
Mwanza siku ya Idd Mosi na Idd pili.
Pia
mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza katika
uwanja wa CCM Kirumba, na mkutano mwingine wa ndani uliofanyika katika
hoteli moja maarufu jijini Mwanza usiku, inadaiwa kwamba aliigharimia
yeye.
Nchemba anadaiwa kulipia gharama za makatibu hao kutoka vituo vyao vya kazi kwa maana ya usafiri na posho.
Mbali
na mkutano wa Mwanza, Nchemba anadaiwa kuwaalika tena makatibu wa CCM
51 mjini Dodoma wakati wa Bunge la Bajeti mwaka huu na kuwagharimia
usafiri, posho na malazi.
Wakati
akilipa gharama hizo, kwa miezi ya Juni na Julai, vyama vya siasa
vilikuwa havijapewa ruzuku na kwa kiasi kikubwa watendaji wote wa CCM
kama walivyo wa vyama vingine vya siasa, walikuwa hawajalipwa mishahara
yao ya Juni na Julai.
Makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya Tanzania Bara kimsingi wanawajibika kiutendaji kwa Nchemba kama Naibu Katibu Mkuu CCM Bara.
Hata
hivyo, akizungumza na NIPASHE katika mahojiano kwa simu jana, alisema
kimsingi kila kazi nzuri inayofanywa na kiongozi inawafanya watu waone
ni harakati za kutaka urais 2015 japo ndiyo kipimo cha kuaminiwa.
“Nilichosema
wakati nahojiwa na kituo cha televesheni nilisema sitangazi, lakini
nafanya kazi niliyopewa ya Naibu Waziri wa Fedha hivyo lazima
nihakikishe bajeti ya serikali inatekelezwa,”alisema.
Nchemba
alisema yeye ni kiongozi wa chama anayepaswa kuwa mfano wa kuheshimu
kanuni na taratibu za chama hivyo hawezi akakurupuka na kutangaza kwamba
atawania urais.
“Mwanza nilifanya mkutano wa hadhara ambao msingi wake ilikuwa ni kusisitiza masuala ya kodi na ajira,”alisema.
Pia
alisema hakulipia gharama za makatibu waliosafiri hadi Mwanza, kwa kuwa
chama kina taratibu za kulipia watendaji wake gharama kama hizo.
Nchemba
anakuwa kiongozi wa pili ndani ya CCM na serikali kutamka hadharani ama
anautaka urais au anasukumwa na watu kujitokeza kuuwania mwaka 2015.
Mwingine
ni Naibu Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, ambaye
alisema kwamba amekwisha kufanya kazi ya kujiandaa kwa asilimia 90 na
kilichobaki ni kuonana na viongozi wa dini tu.
Wapo wanachama kadhaa ambao wameonyesha nia ya kutaka kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM.
Miongoni
mwao ni mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
Akizungumzia
suala la ajira, Nchemba alisema kuna haja kwa wananchi kuachana na
fikra kuwa ajira pekee ni ile ya kuajiriwa serikalini.
Alisema
ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini, halmashauri za wilaya na
majiji zinatakiwa kuhakikisha zinapopima viwanja vya makazi, zinafanya
hivyo kwa kutenga maeneo ya uwekezaji ambako kutajengwa viwanda
vitakavyotoa ajira kwa vijana.
Alitaka
kuwapo na muda maalum kwa mwekezaji anayepewa eneo la uwekezaji na
anaposhindwa kuliendeleza, anyang’anywe na kupewa mwingine.
Alisema
hilo litasaidia kuondokana na tatizo la baadhi ya wawekezaji kuhodhi
maeneo ya uwekezaji na kushindwa kuyaendeleza kwa muda mrefu.
Nchemba
alisema kumekuwa na tatizo la ukosefu wa uadilifu na bidii ya kufanya
kazi kwa baadhi ya wananchi wanaopewa fursa ya kazi.
Alisema hali hiyo wakati mwingine inawafanya wawekezaji hususan nchini, kuchukua hatua ya kuajiri watu kutoka nje ya nchi.
“Kuna
baadhi ya nchi kama Marekani, mfanyakazi anapokuwa kazini, haruhusiwi
hata kuongea na simu au kusoma gazeti. Lakini hapa kwetu watu
hawaonyeshi bidii ya kufanya kazi kwa lengo la kuongeza uzalishaji,” alisema.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

