Mfalme
wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameshindwa kustahimili
msiba wa mkewe, Asha Msindi (34) na kujikuta akizimia msibani wakati wa
maziko, Risasi Jumamosi lina stori ya kusikitisha.
Mwili wa marehemu Asha Mohamed Shiengo 'Mama Tunda' ukiombewa kabla ya mazishi.
Tukio
hilo ambalo liliibua simanzi nzito mkoani hapa na kuweka historia
lilijiri juzi, Alhamisi katika Mtaa wa Amani, Mji Mkuu, alipokuwa
akiishi Asha na mama yake.
Aliyekuwa mke wa Afande Sele, Asha Msindienzi za uhai wake.
RAFIKI AFUNGUKA
Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa Afande, gwiji huyo wa muziki ambaye
alitengana na mkewe mapema mwaka huu, alipopewa taarifa hizo za msiba,
hakuamini hadi alipofika nyumbani kwa marehemu na kukuta watu wamejaa
msibani.
Mfalme wa Rhymes Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ akiwa amezimia msibani.
“Alipigiwa
simu na baadhi ya ndugu wa mke kumueleza habari za msiba, hakushtuka
sana maana hakuwa ameamini moja kwa moja hivyo akasema ataamini
atakapofika msibani na kukuta msiba,” alisema mtu huyo wa karibu ambaye
aliomba hifadhi ya jina gazeti.
Afande Sele akiweka udongo kwenye kaburi la mke wake Mama Tunda.
AZIMIA
Mtu
huyo wa karibu alizidi kueleza kuwa, mara baada ya kufika nyumbani hapo
na kukuta ndugu, jamaa na marafiki wamekusanyika ndipo Afande
alipoanguka na kuzimia kwa takriban saa nne kisha akaziduka.
“Alipofika
pale nyumbani kwa mkewe na kukuta umati ukiwa msibani, alijitahidi
akaingia ndani na alipomuona mama mkwe wake, hapohapo alianguka na
kuzimia,” alisema mtu huyo.
Mama wa marehemu Asha Msindi (34), Hamida Rajab Sulu.
APEPEWA
Rafiki
huyo wa Afande alizidi kueleza kwamba, baada ya kuzimia, ndugu wa mke
walimlaza kwenye kochi kisha baadaye rafiki zake walimchukua na
kumpeleka nyumbani kwake maeneo ya Msufini ambapo walimpepea kisha
wakammwagia maji ya baridi, akazinduka.
Alipozinduka,
aliwaomba marafiki zake wampeleke tena msibani ambapo alipofika aliomba
kuletewa mwanaye mdogo, Asantesanaa, akambeba na kukaa naye msibani
hapo.
Majirani waliofika msibani wakiwa pamoja na mama wa marehemu(Asha Msindi),Hamida Rajab Sulu(wa kwanza kulia).
CHANZO CHA KIFO
Akizungumza
na mwandishi wetu, mama mzazi wa marehemu, Hamida Rajab Sulu, alisema
kuwa mwanaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria kali kwa
takriban siku tatu, ndipo Jumatano iliyopita asubuhi walipompeleka
katika Hospitali ya St. Mary mjini hapa.
Alisema
kuwa alipofikishwa hospitalini hapa alilazwa na kuanzishiwa dozi ya
malaria lakini baadaye hali ilizidi kuwa mbaya wakalazimika kumuhamishia
kwenye Hospitali ya Manispaa ya Morogoro.
“Walimlaza
pale kwa saa kadhaa, walipoona hali inazidi kuwa mbaya, walitushauri
tumuhamishie kwenye Hospitali ya Manispaa Morogoro.“Tulipofika pale
walimuanzishia dripu ya kutibu malaria, kabla hata haijaisha, mgonjwa
alianza kutikisa miguu, hapohapo akafariki dunia. Ilikuwa muda wa saa
5:00 usiku,” alisema mama huyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF', Simon Mwakifwamba akimpa pole Afande Sele.
WASANII WATINGA MSIBANI
Msiba
huo umeacha historia ya aina yake kwani kesho yake asubuhi (Alhamisi),
wasanii wengi walifika msibani hapo kwa ajili ya kuomboleza hali ambayo
iliwafanya baadhi ya watu kushangaa wasanii badala ya kuomboleza.
Picha ya familia: Kutoka
kulia ni Asha Mohammed Shiengo ‘Mama Tunda’ enzi za uhai wake, Selemani
Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.
Miongoni
mwa wasanii ambao walifika mapema msibani hapo ni pamoja na Rais wa
Shirikisho la Filamu Nchini, Simon Mwakifwamba na Joseph Haule ‘Profesa
Jay’.
AFANDE ANENA
Akizungumza
kwa uchungu makaburini hapo, Afande Sele alisema kifo cha mkewe ni pigo
kubwa maishani mwake kwani ndiye aliyekuwa faraja ya pekee kwa wanaye,
Tunda na Asantesanaa.
“Hili ni pigo kubwa maishani mwangu, mama Tunda
alikuwa ndiye kila kitu kwa wanangu, inaniuma sana,” alisema Afande
akitokwa machozi.
Mwanamuziki Profesa Jay (kulia) akimfariji Afande Sele.
AZIKWA
Baada
ya umati kujikusanya msibani hapo, taratibu za mazishi zilifanyika siku
hiyohiyo na wakaelekea kuzika kwenye Makaburi ya Kola mjini hapa.
TUJIKUMBUSHE
Kabla
Afande Sele na mama Tunda hawajatengana mapema mwaka huu, waliishi kama
mume na mke kwa zaidi ya miaka kumi na kufanikiwa kupata watoto wawili,
Tunda na Asantesanaa.