Habari Kali
Loading...

Mfungo wa mwezi wa Ramadhani: Bei za Vyakula Juu jijini Dar

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
BAADHI ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamelalamikia bei kubwa za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye badhi ya masoko jijini humo.
Wakizungumza  kwa nyakati tofauti, wakazi wa jiji hilo Bw. Khamis Mshaka na Bi. Salma Jumbe, walisema baadhi ya wafanyabiashara wanapandisha bei ya vyakula ili kupata faida.
Walisema hali hiyo inawafanya wananchi wengi hasa wenye kipato kidogo washindwe kumudu bei za vyakula wanapokwenda sokoni.
“Tabia hii si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo…bidhaa zilizopo sokoni si za Waislamu pekee, hivyo tunaziomba mamlaka husika zichukue hatua,” walisema.
Bi. Jumbe alisema, baadhi ya wafanya biashara wanaficha vyakula kwenye maghala ili siku zinavyozidi kwenda, waviuze kwa bei kubwa jambo ambalo serikali inapaswa kulifanyia uchunguzi ili kukomesha tabia hiyo.
mihogo
Kwa upande wake, Bi.Maria Albert ambaye ni mamalishe, anayefanya biashara ya kuuza chakula kwenye Mtaa wa Kongo, Kariakoo, alisema kutokana na bei kubwa ya vyakula, wanashindwa kupata faida.
Kutokana na malalamiko hayo, Mpekuzi ilitembelea kwenye baadhi ya masoko kama Kariakoo, Buguruni, Tandika, Ilala, Kisutu na kubaini baadhi ya wafanyabiashara wanauza vyakula kwa bei kubwa. Bw. Ally Gumbo ambaye ni mfanyabiashara wa mihogo, viazi na magimbi katika Soko la Kariakoo, alisema bei ya mihogo na magimbi imepanda kutokana na kupandishiwa bei na wakulima.
Alisema bei ya sasa kwa mhogo mmoja ni kuanzia sh .1,000 kutokana na ukubwa wake ambapo magimbi ni sh. 3,000 kwa sado moja tofauti na awali ambapo ilikuwa ni sh.1, 500.
Naye Bw. Brown Sanga, mfanyabiashara wa nafaka katika Soko la Kisutu, alisema ni dhambi kupandisha bei za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani.
“Wafanyabiashara tunapaswa kuwa na ubinadamu hata kama tunatafuta pesa, tunatakiwa kusaidiana ili ndugu zetu Waislamu tusiwaweke katika mazingira magumu ya kutafuta futari,” alisema.
Hali katika kampini ya RJ inayoongozwa kwa ubiya kati ya Vicent Kigosi ( Ray) na Blandina Chagula ‘Johari’, inazidi kuwa tete kwa kile kinachoelezwa kuwa johari hataki kufanya kazi pamoja na ‘mke mwenza’  Chuchu Hans.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu na wasanii hao kilisema kuwa mwezi mmoja uliopita Johari na Chuchu, walikuwa katika kuelekea kuelewana ambapo johari, alishakubali yaishe kuwa Ray wake ameshapokonywa na mtoto huyo wa Kitanga .
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa baada ya Johari kuwa katika hali hiyo,ndipo Chuchu alipoanza kutanua makucha yake ndani ya kampuni kwa kujifanya ni mmoja kati ya wakurugenzi wakati ukweli haupo hivyo.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa imefikia hatua Chuchu, kaanza kutoa amri kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo bila ya kupata kibali kutoka kwa wakurugenzi waasisi ambao mtaji wao unadaiwa kutokana na  Johari ‘kumpiga’ changa la macho mfanyabiashara maarufu kutoka mkoani Mbeya.
Mpashaji huyo alizidi kusema kuwa bifu liliibuka upya mkoani Dodoma, ambako Ray na Johari walikwenda katika ziara ya Kilimanjaro Music Awards Tour, na mashabiki wao kuwataka wapande jukwaani kwa pamoja.
Mtoa habari hiyo alisema kuwa kuwa kutokana na hali hiyo, ndipo Chuchu alipoanzisha bifu la chinichini lililopelekea hadi sasa kwenye kampuni hiyo kuzuka mtafaruku mkubwa huku Johari, akitaka kujitenga kabisa na Ray lakini kinachomkwamisha ni pesa zake nyingi alizowekeza.
Inadaiwa  kuwa Johari amekuwa mkali sana sasa hivi akimtaka mkurugenzi mwenzake Ray, wagawane kila kitu mpaka nguo za ndani walizonunua kwa pesa za kampuni yao hiyo.
Katika kufuatilia habari hizo ili kupata ukweli kuhusiana na timbwili hili mwanahabari wetu aliwasaka wote kwenye simu zao za mkononi, lakini wote hawakutaka kutoa ushirikiano kwa kile walichokieleza kuwa wapo bize na maswala binafsi.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top