Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Mkimbizi wa Kisomali mwenye asili ya Kibantu, Ramadhani Haji katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo ambao waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania.
Kulia kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu (hawapo pichani), baada ya kutoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Kulia (Meza Kuu) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima (wapili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu baada ya kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania.Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu wanaoishi katika Makazi ya Chogo, Handeni mkoani Tanga wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo pichani) alipofika katika makazi yao ili kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika makazi hayo baada ya kuomba uraia kwa mujibu wa sheria ya Tanzania. Waziri Chikawe alitoa vyeti kwa wakimbizi hao na kuwataka kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

